Pata taarifa kuu

Lampard ateuliwa tena kuinoa Chelsea kwa muda

NAIROBI – Frank Lampard ameteuliwa kuwa meneja wa muda wa klabu ya Chelsea inayoshirki katika ligi kuu ya Uingereza hadi mwisho wa msimu.

Frank Lampard, mchezaji wa zamani wa Cheslea
Frank Lampard, mchezaji wa zamani wa Cheslea Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kuteuliwa kwake inakuja ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu atimuliwa na klabu hiyo kwa kile kilitajwa kuwa matokeo duni.

Lampard mwenye umri wa miaka 44, Mchezaji wa zamani ambaye pia ndiye mfungaji bora katika klabu hiyo, anachukua nafasi hiyo baada ya Graham Potter kufutwa kazi kutokana na matokeo duni.

Kocha huyo aliwahi kuionoa Chelsea kati ya mwezi Julai mwaka wa 2019 hadi mwezi Januari mwaka wa 2021.

Aidha mchezaji huyo wa zamani alitimuliwa kutoka katika klabu ya Everton kutokana na kile kilitajwa na uongozi wa klabu hiyo kama makubaliano na pande zote.

Kwa sasa Chelsea wako katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na mechi wikendi hii dhidi ya Wolves ugenini.

Kwa mujibu wa wamiliki wenza wa Chelsea, Todd Boehly na Behdad Eghbali, Lampard atachukua majukumu ya klabu hiyo wakati huu wakiwa katika mikakati ya kumtafuta kocha wa kudumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.