Pata taarifa kuu

Patrick Vieira ametimuliwa Crystal Palace

NAIROBI – Klabu ya Crystal Palace inayoshiriki katika ligi kuu ya Uingereza, imethibitisha kutimuliwa kwa meneja wake Patrick Vieira siku ya Ijumaa huku klabu hiyo ikikabiliwa na hatari ya kushuka daraja katika Ligi ya Premia baada ya kuandikisha matokeo mbaya.

Aliyekuwa kocha wa Crystal Palace Patrick Vieira
Aliyekuwa kocha wa Crystal Palace Patrick Vieira POOL/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Parish, wamechukua hatua hiyo kwa masikitiko makubwa ila kutokana na matokeo ya miezi ya hivi karibuni yameweka klabu hiyo  katika hali mbaya kwenye ligi .

Aidha Palace imesema kuwa wamechukua uamuzi huo kama njia moja ya kurejesha hadhi ya timu na kuiweka katika nafasi bora ilikuepuka kushushwa daraja.

Klabu hiyo kwa sasa inashikilia nafasi ya 12 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza na kwa sasa imeanzisha mchakato wa kumteua kocha mwengine kuchukua nafasi ya Vieira.

Wanachama watatu na wafanyakazi wa ukufunzi wa Vieira, Osian Roberts, Kristian Wilson na Said Aigoun nao pia wameondoka Selhurst Park.

Palace haijashinda  mchezo wowote mwaka 2023 chini ya kiungo huyo wa  zamani wa Arsenal na Ufaransa Vieira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.