Pata taarifa kuu

Achraf Hakimi ashtakiwa kwa tuhuma za ubakaji

NAIROBI – Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wamethibitisha kuwa mchezaji wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Morocco Achraf Hakimi,ameshtakiwa na kosa la ubakaji.

Achraf Hakimi, Mchezaji wa PSG
Achraf Hakimi, Mchezaji wa PSG DeFodi Images via Getty Images - DeFodi Images
Matangazo ya kibiashara

Hakimi, mwenye umri wa miaka 24, amehojiwa na waendesha mashataka siku ya Alhamis kwa tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka 24 na baadae kufunguliwa mashtaka.

Mchezaji huyo mzawa wa Madrid, alichangia pakubwa katika mafanikio mazuri ya timu ya taifa ya Morocco katika mashindano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana na ameonekana Ijuma asubuhi akifanya mazoezi na klabu yake ya PSG.

Hadi tukichapisha taarifa hii, Klabu yake haikuwa imetoa taarifa kuhusu madai haya.

Hakimi anatuhumiwa kumlipia nauli mwanadada husika  kama njia moja ya kusafiri hadi nyumbani kwake wakati mke wake na watoto wakiwa katika likizo.

Kwa mujibu wa sheria za Ufaransa, kushtakiwa haimanishi kwamba kesi hiyo itasikilizwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.