Pata taarifa kuu

NBA: LeBron James aweka rekodi ya mfungaji bora wa muda wote

Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini Marekani mwenye asili ya Kiafrika, LeBron James, usiku wa kuamkia leo ameweka rekodi yakuwa mchezaji wa kwanza wa ligi ya NBA kufunga alama nyingi zaidi, akimpiku Kareen Abdul-Jabbar, aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo kwa miaka 39.

LeBron James, mchezaji wa Los Angeles Lakers. Feb 8, 2023
LeBron James, mchezaji wa Los Angeles Lakers. Feb 8, 2023 AP - Mark J. Terrill
Matangazo ya kibiashara

 

James anayechezea klabu ya Los Angeles Lakers, alifunga alama 38 katika ushindi wa vikapu 133 dhidi ya 130 vya Oklahoma City.

Abdul-Jabbar ambaye pia aliwahi kuchezea Lakers, aliweka rekodi hii April mwaka 1984, miezi nane kabla "King James" hajazaliwa.

"Kuwa na uwezo wa kufikia rekodi hii mbele ya nguli Kareem, ni jambo lenye maana kubwa kwangu," alisema James.

Baada ya kufikia rekodi hiyo, James alishangilia kwa kutanua mikono yake katika kuzunguka dimba la Crypto.Com, wakati akifikisha ushindi wa alama 38,388.

Abdul-Jabbar aliyekuwa uwanjani kufuatilia mchezo huo, alikuwa miongoni mwa watu wa awali kabisa kumpingeza James, ambapo hata mchezo ulisimama kwa shangwe kumpongeza mchezaji huyo.

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.