Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA- MICHEZO

Vincent Aboubakar ameondoka Al-Nassr ya Saudi Arabia

Mshindi mara tano wa tuzo la Ballon d’or, Cristiano Ronaldo, sasa atapata nafasi ya kuichezea Al-Nassr kwa mara ya kwanza.

Vincent Aboubakar, wa Cameroon
Vincent Aboubakar, wa Cameroon Β© AFP - KENZO TRIBOUILLARD
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya klabu hiyo ya Saudia kusitisha kandarasi ya mshambuaji matata Vincent Aboubakar.

Aboubakar, raia wa cameroon ataondoka katika klabu hiyo ili kutoa nafasi kwa Ronaldo, kwani sheria za ligi ya Saudia zinasema kuwa vilabu vinaweza tu kusajili hadi wachezaji wanane wa kigeni kwa kila kikosi.

Kulingana na ripoti kutoka Ufaransa, Aboubakar alikubali kuvunja mkataba wake na atalipwa fidia na klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba Wake.

Kuondoka kwake kunamaanisha kuwa Ronaldo anaweza kucheza mechi yake ya kwanza inayotarajiwa kuchezwaΒ Januari 22.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 lazima amalize adhabu ya kutocheza mechi mbili baada ya kugonga simu ya mkononi kutoka kwa mikono ya kijana wa miaka 14. Kijana huyo alikua ni shabiki aliyehudhuria mechi baina ya Manchester United na Everton mwaka uliopita 2022.

Ronaldo hajacheza mchezo wowote wa ushindani tangu aliposhiriki akitokea benchi katika mchezo wa robo fainali kwenye Kombe la Dunia dhidi ya Morocco mnamo Desemba 10.

Β 

Na Paul Nzioki

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.