Pata taarifa kuu
AUSTRALIA- TENNESI

Venus Williams amejiondoa mashindano ya Australian Open

Mshindi wa saba wa Grand Slam, Venus Williams mwenye umri wa  miaka 42 amejiondoa katika mashindano ya Australian Open yatakayoanza baadaye mwezi huu kutokana na jeraha kwenye mechi za kujifua. Venus alipata jeraha hilo katika mashindano ya ASB Classic jijini Auckland.

 Venus Williams mchezaji wa tenisi
Venus Williams mchezaji wa tenisi GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Venus hajawai kushinda taji la Australian Open licha ya kufika fainali mbili mwaka 2003 na 2017.

Kuna hofu pia ikiwa raia wa Poland Iga Swiatek – mshindi wa Grand Slam mara tatu - atashiriki Australian Open baada ya kujiondoa kwenye mashindano ya Adelaide 2 WTA 500 yatakayoanza wiki ijayo kufuatia jeraha la bega.

Ni suala la kusubiri kubaini iwapo Emma Raducanu anayeorodheshwa wa kwanza duniani atashiriki au la baada ya muingereza huyo kupata jeraha la kifundo cha mguu siku ya Alhamisi katika mashindano ya ASB Classic.

Kwa upande wa wanaume, bingwa wa dunia Carlos Alcaraz naye pia hatoshiriki kufuatia jeraha la mguu katika mazoezi ya kabla ya msimu kuanza.

Raia huyo wa Uhispania mwenye umri miaka 19 aliandikisha rekodi ya mchezaji mchanga zaidi upande wa  wanaume kwa  kuorodheshwa nambari moja duniani baada ya kushinda taji la kwanza la Grand Slam mwezi Septemba mwaka 2022 katika mashindano ya US Open.

Pengo lake lina maana kuwa muhispania mwenzake Rafael Nadal ambaye ndiye bingwa mtetezi atalenga kuchukua nafasi ya bingwa wa dunia ugani Melbourne Park.

 

Na Jaysen Sagini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.