Pata taarifa kuu
CAMEROON-MICHEZO-TANZIA

Mchezaji wa zamani wa Cameroon Modeste M’Bami amefariki

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon Modeste M’Bami amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 40.

Modeste M'Bami,Mchezaji wa zamani wa Cameroon
Modeste M'Bami,Mchezaji wa zamani wa Cameroon AFP - MARTIN BUREAU
Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo alishinda dhahabu katika Michezo ya Olimpiki akiwa na nchi yake mwaka wa 2000. Baadaye alijiunga na vilabu viwili vikubwa vya Ufaransa huko PSG kati ya 2003 na 2006, na Marseille kwa misimu mitatu iliyofuata.

M’Bami pia alishinda kombe la Coupe de France mara mbili akiwa na Parisians.

Aliondoka Ufaransa baada ya kukaa kwa miaka tisa na kuhamia Uhispania kuichezea Almería kwa misimu miwili. Kabla ya kustaafu alirejea Ufaransa na Le Havre mnamo 2015.

Aliaga dunia bado akiwa anaishi katika jiji la Le Havre. Ndani ya miaka tisa amecheza mechi 37 kama mchezaji wa kimataifa wa Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.