Pata taarifa kuu
CHAN 2023

CHAN 2023: Morocco na DR Congo zajipanga

Na: Jason Sagini

CHAN 2023, nchini Algeria
CHAN 2023, nchini Algeria © CAF on line
Matangazo ya kibiashara

Mashindano ya mataifa ya Afrika yanayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani maarufu CHAN, yatang’oa nanga Ijumaa wiki ijayo nchini Algeria.

Morocco na DR Congo zinashikilia rekodi ya timu zenye mafiniko makubwa kwenye historia ya mashindano kwa kushinda mataji mawili kila mmoja. Nini kinachoendelea kwenye kambi ya timu hizi zinapolenga kushinda taji la tatu ?

Timu ya taifa ya DRC Leopard
Timu ya taifa ya DRC Leopard © CAF

Leopard inaonekana timu yenye masaibu na vidonda kuelekea mashindano baada ya kukumbwa na matatizo ya fedha. Baada ya kocha Otis Ngoma kuonyesha matumaini makubwa kutwaa taji la tatu, Imani hiyo imeshuka baada ya kocha huyo kudai yeye si kocha rasmi wa timu ya taifa.

Mwalimu Otis amejitokeza na kudai hajatia saini kandarasi rasmi na shirikisho la mpira wa miguu nchini DRC  kwa sababu mkataba aliotia saini bado haijathibitishwa na rais wa shirikisho hilo Jean Blaise Mayolas.

Fauka ya hayo, Ngoma ameonyesha kugadhabika kwake kwani wachezaji hawajapokea marupurupu yao katika mechi za kirafiki ambazo wamecheza zaidi ya mwezi mmoja.

DR Congo washindi wa mwaka 2016 wamepangwa katika  kundi moja na Ivory Coast, Senegal na Uganda.

Mabingwa watetezi Morocco nao wamejiandaa vipi?

Wachezaji wa timu ya taifa ya Morocco wakati wa mashindano yaliyopita
Wachezaji wa timu ya taifa ya Morocco wakati wa mashindano yaliyopita FADEL SENNA / AFP

Shirikisho la soka nchini Morocco limetishia kujiondoa kwenye mashindano ikiwa Algeria haitawaruhusu kusafiri moja kwa moja kutoka Rabat hadi jiji la Constantine linaloandaa mashindano. Algeria na Morocco ni mataifa jirani kaskazini magharibi mwa bara Afrika.

Uhusiano chachu ulizuka kati ya mataifa haya tangu kupatikana kwa uhuru kutokana  na Algeria kuunga mkono Polisario – ambalo ni vuguvugu la waasi la kabila la Sahrawi linalodai umiliki wa eneo la Sahara magharibi.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2021, Algiers ilikata mahusiano yote na Rabat kupelekea kufunga anga yake kwa ndege zote za Morocco kufuatia kukatika kwa uhusiano wao wa kidiplomasia. Mpaka kati ya mataifa haya mawili umesalia kufungwa tangu mwaka 1994.

Zimesalia siku sita michuano kuanza, kinachostaajabisha shirikisho la soka barani Afrika CAF ingali kupokea ripoti kuhusu mgogoro huu.

Morocco tayari imewasilisha kikosi cha mwisho ambacho kinahusisha wachezaji ambao wamezaliwa kuanzia mwaka 2000. Simba hao wa Atlas wamo kwenye kundi moja na Sudan, Madagascar na Ghana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.