Pata taarifa kuu
UFARANSA-ARGENTINA-MICHEZO

Mashabiki wa Ufaransa Wataka Fainali ya Kombe la Dunia 2022 Kurudiwa

Na Paul NziokiIkwia imepita wiki moja  baada ya Argentina kushinda ubingwa wa Dunia katika mpira wa miguu kwa wanaume.Mashabiki wa timu ya taifa ya Ufaransa wanataka mechi ya fainali kurudiwa. 

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na Argentina kabla ya mechi ya fainali nchini Qatar
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na Argentina kabla ya mechi ya fainali nchini Qatar REUTERS - PAUL CHILDS
Matangazo ya kibiashara

Jukwa moja mtandaoni limekusanya zaidi ya saini laki mbili kuunga mkono ombi la kutaka fainali hiyo irudiwe. 

Mashabiki hao wa Ufaransa, wanarejelea Ángel Di María alivyochezewa visivyo na Ousmane Dembélé na mwamuzi akatoa penalti iliyofungwa na Lionel Mesii.Kwa mujibu wao Mbappe alifanyiwa madhambi mwanzoni mwa hatua iliyopelekea Argentina kufunga bao la pili.

Kulingana na Gazeti la THE MIRROR, Ombi hilo tayari ni miongoni mwa 20 bora kwenye MesOpinions, jukwaa lililotumiwa kwa kampeni hiyo. Iwapo itazidi saini nusu milioni itaingia kwenye tatu bora.

Mashabiki waliotoa saini zao wameeleza kero zao na kumshutumu mwamuzi pamoja na kuwaita wachezaji wa  Argentina kuwa "tapeli".

Miongoni mwa wachezaji wanaongoza kwa kushutumiwa ni Mlinda lango Emiliano Martinez aliyeokoa penalti ya Kingsley Koman.

Hali hii huenda ikazua tumbo joto miongo mwa wafuasi wa soka nchini Ufaransa haswa Mashabiki wa PSG wakati huu Messi anapotarajiwa kurejea PSG kwa ajili ya mechi za msimu wa 2022-23. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.