Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA 2022-SENEGAL

Senegal yafuzu hatua ya 16 michuano ya kombe la dunia

Timu ya taifa ya soka ya Senegal kwa jina maarufu, Simba wa Teranga, wameleta furaha kwa mashabiki wa soka barani Afrika, baada ya kufuzu katika hatua ya 16 bora, katika harakati za kuwania kombe la dunia, michuano inayoendelea nchii Qatar.

Wachezaji wa Senegal wakisherehekea ushindi dhidi ya Ecuador, wa mabao 2-0 na kufuzu katika hatua ya mwondoano, 29/11/2022
Wachezaji wa Senegal wakisherehekea ushindi dhidi ya Ecuador, wa mabao 2-0 na kufuzu katika hatua ya mwondoano, 29/11/2022 REUTERS - JENNIFER LORENZINI
Matangazo ya kibiashara

Hii ilikuja baada ya Senegal kuifunga, Ecuador bao 2-1 katika mechi za kutamatisha kundi A, siku ya Jumanne.

Ismaila Sarr alikuwa wa kwanza, kuipa Senegal bao kupitia mkwaju wa penalty katika dakika ya 44 lakini Moises Caicedo, akaisawazishia Ecuadoe katika dakika ya 67 ya mchezo, lakini dakika tatu baadayeΒ alirejesha furaha baada ya kufunga kwa kichwa, bao ambalo liliwapa ushindi wawakilishi hao wa Afrika.

Senegal imekuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufuzu katika hatua hiyo, tangu michuano ya mwaka 2014.

Kalidou Koulibaly akisherehekea baada ya kufunga bao
Kalidou Koulibaly akisherehekea baada ya kufunga bao REUTERS - DYLAN MARTINEZ

Timi nyingine iliyofuzu katilka hatua hiyo kutoka kundi A, ni Uholanzi , baada ya kuwafunga wenyeji Qatar mabao 2-0 na kuongoza kundi hilo kwa alama saba.

Katika matokeo ya kutamatisha kundi B, Uingereza na Marekani zimefuzu pia.

Marekani iliifunga Iran bao 1-0, lillofungwa naΒ katika dakika ya 38 ya mchuano huo uliojawa pia hisia za kisiasa kati ya nchi hizo mbili.

Christian Pulisic mshambuliaji wa timu ya Marekani
Christian Pulisic mshambuliaji wa timu ya Marekani GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP

Uingereza nayo, iliishinda Wales mabao 3 kwa 0 na kuongoza kundi hilo kwa alama saba.

Leo, ni zamu ya kundi C, Poland watamenyana na Argetina, timu zote zikisaka nafasi ya kufuzu, lakini Saudi Arabia ambayo pia ina nafasi ya kusonga mbele itacheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Mexico.

Katika kundi D, wawakilishi wengine wa Afrika, Tunisia ambayo haina matumaini ya kusonga mbele itacheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Ufaransa ambayo tayari imeshafuzu.

Australia ambayo ina alama tatu katika kundi hilo, itachuana na Denmark.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.