Pata taarifa kuu

Pazia la michuano ya kombe la dunia lafunguliwa nchini Qatar

Michuano ya kombe la dunia nchini Qatar imeanza kwa shamrashamra katika hafla ya kihistoria. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa la Mashariki ya Kati kuandaa michuano ya kombe la dunia.

Mwanasoka wa zamani wa Brazil Roberto Carlos, bingwa wa dunia mwaka wa 2002, akionyesha Kombe la Dunia mnamo Novemba 19, 2022 nchini Qatar.
Mwanasoka wa zamani wa Brazil Roberto Carlos, bingwa wa dunia mwaka wa 2002, akionyesha Kombe la Dunia mnamo Novemba 19, 2022 nchini Qatar. REUTERS - MOLLY DARLINGTON
Matangazo ya kibiashara

Qatar imekabiliwa na ukosoaji mwingi na kutia doa sifa yake ya kuandaa michuano ya kombe la dunia.

Qatar imekosolewa juu ya masuala ya haki za wafanyakazi wa kigeni, watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na haki za kijamii. Nchi hiyo pia ilitangaza kupiga marufuku unywaji wa pombe viwanjani.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa ambao wamewasili Doha kushiriki hafla hiyo ya ufunguzi kabla ya mechi ya kwanza baina ya wenyeji Qatar na Ecuador. Viongozi wengine wanaohudhuria ufunguzi ni pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, rais wa Algeria, Rais wa Senegal, Rais wa Mamlaka ya Palestina pamoja na rais wa Rwanda Paul Kagame. 

Baadhi ya wachezaji wameripotiwa kwamba hawataweza kushiriki kutokana na kuwa majeruhi, hali inayochangia kupunguza msisimko wa michuano hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.