Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA 2022

Kombe la dunia kuanza Jumapili nchini Qatar, maandalizi yakamilika

Maandalizi yamekamika nchini Qatar kuelekea kuanza kwa michuano ya kombe la dunia katika mchezo wa soka, kuanzia hapo kesho.

Rais wa Shirikisho la soka duniani  FIFA, Gianni Infantino akizungumzia maandalizi ya michuano ya kombe la dunua, Novemba 19 2022 jijini Doha
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino akizungumzia maandalizi ya michuano ya kombe la dunua, Novemba 19 2022 jijini Doha AP - Abbie Parr
Matangazo ya kibiashara

Wakati zikisalia saa chache, kuelekea mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Qatar na Ecuador, kesho jioni, rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino ameyashtumu mataifa ya Magharibi kwa unafiki, kuhusu madai ya rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Infatino, ametetea hatua ya Qatar kuwa wenyeji wa michuano hii mikubwa, katika kipindi hiki ambacho taifa hilo la Kiarabu limekuwa likidaiwa kuminya haki za wafanyakazi wa kigeni, wanawake na wapenzi wa jinsia moja.

Aidha, amesema elimu inayatolewa kuhusu maadili, inaegemea upande mmoja na ni unafiki kutoka kwa mataifa ya Magharibi.

Kwa upande wake, Qatar inasema inalengwa na kubaguliwa na kujitetea kuwa imeimarisha sekta ya kufanya kazi na kuorodheshwa kufanya vema kwenye ukanda huo wa Mashariki ya Kati.

Katika hatua nyingine, waandalizi wa michuano hii, wamepiga marufuku uuzwaji wa pombe katika viwanja vitakavyoandaa michuano hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.