Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA- MANCHESTER UNITED

Ligi kuu Uingereza: Hatima ya Cristiano Ronaldo ugani Old Traford

Mshambuliaji wa timu ya Manchester United inayoshiriki katika ligi kuu ya Uingereza Cristiano Ronaldo bado anataka kuondoka katika timu hiyo ingawa hatima yake bado haijajulikana baada ya mazungumzo marefu wiki hii.

Cristiano Ronaldo.
Cristiano Ronaldo. AP - Dave Thompson
Matangazo ya kibiashara

Ronaldo amesema kuwa bado ana kiu ya kucheza katika klabu bingwa bara ulaya na vile vile kushiriki katika kutetea mataji makubwa na licha ya haya yote, United haitaki kumwachilia aondoke Old Traford.

Raia huyo wa Ureno aidha amedokeza kuwa atarejea katika timu ya Manchester United wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano ya Uhispania siku ya Jumapili. Haya ni kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii ambao aliandika, “Jumapili, mfalme atacheza”

Hata hivyo Ronaldo hakujumuishwa kwenya kikosi cha wachezaji 21 ambacho kitacheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Atletico Madrid leo kule Oslo.

Ronaldo na wakala wake Jorge Mendes walikuwa na mkutano na Manchester United mjini Carrington siku ya Jumanne licha ya kukosa mechi za kujipima nguvu kule Thailand na Australia kutokana na maswala ya familia.

Kwa sasa nafasi yake ni finyu sana katika timu ambazo zilionyesha nia ya kumsajili kama vile Chelsea ambayo imeshakata tamaa ilhali Bayern Munich na Atletico Madrid wakitangaza waziwazi kuwa hawamwitaji. Siku ya Jumatano, mashabiki wa Atletico walikuwa na mabaongo uwanjani ambayo yalikuwa na maandishi, “CR7 haujakaribishwa.”

Na George Ajowi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.