Pata taarifa kuu
TENNIS

Bingwa wa mchezo wa Tennis duniani  Ashleigh Barty astaafu

Bingwa nambari moja duniani  katika mchezo wa Tennis kwa upande wa wanawake Ashleigh Barty ametangaza kustaafu.

Ashleigh Barty wakati akicheza Tennis kabla ya kutangaza kustaafu
Ashleigh Barty wakati akicheza Tennis kabla ya kutangaza kustaafu AFP
Matangazo ya kibiashara

Barty raia wa Australia mwenye umri wa miaka 25, ametoa tangazo hilo ambalo halikutarajiwa, akisema ametimiza ndoto yake katika mchezo huo na hana nguvu tena ya kuendelea.

Amechukua hatua hii baada ya kushinda taji la Australian Open, mashindano yalifanyika mwezi Januari.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, akionekana na rafiki yake na mchezaji mwenzake Casey Dellacqua, walioshirikiana katika mchezo huu, amesema muda wake wa kuachana na mchezo huo baada ya kushinda taji la Wimbledon mwaka 2021.

“Mafanikio kwangu ni kufahamu kuwa, nilitoa na kufanya nilichoweza.Nimeridhika.Nimefurahi, “ amesema.

“Sina tena nguvu za kuendelea, sina kingine cha kutoa au kuonesha,” ameongeza.

Mwaka 2019 alishinda taji la French Open na akafanya hivyo mwaka 2021 wakati aliponyakua ubingwa wa taji la Wimbledon, na kuwa miongoni mwa mataji 15 aliyoshinda baada ya kushiriki kwenye mashindano mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.