Pata taarifa kuu
MICHEZO-SOKA

AFCON 2022: Mali yaibwaga Tunisia, refa atupiwa lawama

Timu ya Mali imeifunga Tunisia 1-0 Jumatano hii Januari 12 huko Limbé katika kundi F katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2022). Tunisia imekosa penalti.

Ibrahima Traore akishangilia bao lake la penalti dhidi ya Tunisia.
Ibrahima Traore akishangilia bao lake la penalti dhidi ya Tunisia. © Pierre René-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji na mashabiki wa Tunisia wamekasirishwa na mwamuzi mechi yao dhidi ya Mali Janny Sikazwe kutoka Zambia amemaliza mchezo kabla ya kumalizika kwa muda wa dakika 90 za mchezo. Zaidi ya dakika 40 baada ya kipenga cha mwisho, mechi iliombwa iendelee lakini Tunisia walikataa kurejea uwanjani.

Janny Sikazwe ameweka historia katika michuano hii inayoendelea nchini Cameroon kwa kumalizi mchezo kabla ya kumalizika kwa muda wa dakika 90 za mchezo.

Kosa la kuchezesha mwamuzi Janny Sikazwe, mwishoni mwa Tunisia-Mali, katika kundi F la CAN 2022. Mzambia huyo alipuliza kipenga cha mwisho katika dakika ya 85, bila kujali muda uliopotea.

Haijajulikana ikiwa Tunisia itachukuliwa vikwazo au la na taasisi husika baada ya kususia kurejea uwanjani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.