Pata taarifa kuu
AUSTRALIAN OPEN

Novak Djokovic aruhusiwa kushiriki Australian Open bila kupata chanjo

Mjadala umezuka katika medani ya mchezo wa Tennis duniani, baada ya bingwa mtetezi wa mashindano ya Australian Open kwa upande wa wanaume Novak Djokovic kuruhusiwa kutetea taji lake, bila kupata chanjo dhidi ya virusi vya Covid 19, ambalo ni sharti muhimu kushiriki kwenye mashindano hayo.

Novak Djokovic hajathibitisha iwapo atashiriki kwenye michezo ya  Australian Open kuanzia Januari 17 2022
Novak Djokovic hajathibitisha iwapo atashiriki kwenye michezo ya Australian Open kuanzia Januari 17 2022 OSCAR DEL POZO AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Craig Tiley, Mkuu wa mashidano hayo yanaanza kutifua vumbi Januari 17, amesema Djokovic raia wa Serbia ni miongoni mwa wachezaji na maafisa wachache wapatao 26 walipata kibali cha kushiriki kweye michezo hiyo bila ya kupata chanjo baada ya ombi lao kukubaliwa na jopo la madaktari.

Aidha, ameeleza  kibali kama hiki hutolewa kwa mwombaji kwa sababu binafsi za kiafya ambazo hazijawekwa wazi.

Suala hili limezua mjadala nchini Australia huku raia wa nchi hiyo wakishtumu hatua hiy katika nchi ambayo asilimia 90 ya watu wamepata chanjo.

Djokovic ambaye hajathibitisha iwapo atashiriki katika michuano hiyo, hajaweka wazi pia iwapo amechanjwa au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.