Pata taarifa kuu
KLABU BINGWA-SHIRIKISHO

Klabu bingwa Afrika: Al Ahly na Mamelodi Sundowns wakutana tena hatua ya makundi

Mabingwa wa taji la soka, klabu bingwa barani Afrika, Al Ahly ya Misri, wamepangwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa msimu wa wanne mfululizo, kuwania taji hilo baada ya kufanyika kwa droo jijini Cairo nchini Misri.

Taji la klabu bingwa Afrika
Taji la klabu bingwa Afrika © REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Mbali na Mamelodi Sundowns Ahly ambao wanashikilia rekodi ya kushinda taji hili mara 10, wamepangwa katika kundi la A na klabu kutoka Sudan Al Hilal  na  Al Merrikh.

Kundi B, kuna mabingwa wa taji la ShirikishoRaja Casablanca ya Morocco,  Horoya ya  Guinea, ES Setif kutoka Algeria na AmaZulu. wanaoshiriki katika hatua ya makundi  kwa mara ya kwanza.

Kundi C , kuna  Esperance na  Etoile du Sahel kutoka Tunisia CR Belouizdad ya Algeria na  Jwaneng Galaxy kutoka  Botswana.

Kundi D, kuna mabingwa wa mwaka 2017Wydad Casablanca, kutoka Morocco, Zamalek ya Misri, Petro Atletico na Sagrada Esperanca zote kutoka Angola.

Mechi hiZo zitaanza kuchezwa katikakati ya mwezi Februari.

 

Taji la Shirikisho

  • Kundi A: Pyramids (Misri), CS Sfaxien (Tunisia), Zanaco (Zambia), Al Ahly Tripoli (Libya)
  • Kundi B: JS Kabylie (Algeria) or Royal Leopards (Eswatini), Orlando Pirates (Afrika Kusini), JS Saoura (Algeria), Al Ittihad (Libya)
  • Kundi C: TP Mazembe (DR Congo), Cotonsport (Cameroon), Al Masry (Misri), AS Otoho (Congo Brazzaville)
  • Kundi D: Renaissance Berkane (Morocco), Simba (Tanzania), Asec Mimosas (Ivory Coast), US Gendarmerie (Niger)
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.