Pata taarifa kuu
FIFA-KOMBE LA DUNIA

Infantino asisitiza mabadiliko ya kuhusu muda wa kombe la dunia

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino amesema kubadilisha kipindi cha kufanyika kwa michuano ya kombe la dunia, kutoka miaka minne hadi miwili, kutakuwa na manufaa makubwa ya kifedha kwa vyama vya mchezo huo duniani.

Rais wa Fifa Gianni Infantino
Rais wa Fifa Gianni Infantino Carlos PARRA ANFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Infatatino amesema anatumai mpango huo utawekewa vikwazo na kucheleweshwa na Shirikisho la soka barani Ulaya na Amerika Kusini, wanazopinga mabadiliko hayo.

Rais huyo wa FIFA, katika mkutano na marais wa soka duniani kupitia kwa njia ya mtandao, hata hivyo hakusema iwapo mabadiliko hayo yatapigiwa kura wakati wa mkutano mkuu utakaofanyika tarehe 31 mwezi Machi 2022.

Soma zaidi hapa

Tayari Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limeshaweka wazi kuwa inaunga mkono mabadiliko hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.