Pata taarifa kuu
TENNIS-CHINA

Kutoonekana kwa Peng Shuai kwazua wasiwasi wa Kimataifa

Nchini China, kutoweka kwa mchezaji wa mchezo wa Tennis mwanadada Peng Shuai kunaendelea kuzua maswali mengi kuhusu aliko na usalama wake.

Mchezaji wa Tennis kutoka nchini China Peng Shuai
Mchezaji wa Tennis kutoka nchini China Peng Shuai Philippe HUGUEN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Peng mwenye umri wa miaka 35, na bingwa wa zamani wa dunia wa mchezo huu katika kitengo cha Doubles, haijaonekana kwa wiki tatu sasa, baada ya kudai kunyanyaswa kimapenzi na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu wa China Zhang Gaoli. 

Madai hayo aliyatia kwenye mtandao wa kijamii wa Weibo, Novemba tarehe 2 na baadaye chapisho lake liliondolewa na mtandao huo, lakini wanaharkati wakafanikiwa kuyapisha madai hayo katika mtandao wa Twitter ambao umezuiwa huko China.

Kufuatia hatua hii, wachezaji wenzake wakiongozwa na  Naomi Osaka  na Serena Williams walishtumu kilichompata mchezaji mwenzake na kutaka uchunguzi wa kina kufanyika ili kufahamu alicho mwenzao;

Shirikisho la mchezo wa Tennis kwa upande wa wanawake, limesitisha mashindano yote ya mchezo huo nchini China, mpaka hali ya Peng Shuai itakapobainika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.