Pata taarifa kuu
BRAZIL-SOKA

Mechi ya Brazil na Argentina yasitishwa ghafla, Fifa yataka vikwazo kuchukuliwa

Brazil haikuweza kulipiza kisasi dhidi ya Argentina baada ya mchuano wa fainali ya Copa America kusitishwa ghafla, baada ya maafisa wa afya kuagiza mechi hiyo isitishwe.

Nyota wa Brazil Neymar Jr na wa Argentina wanaongea kabla ya mechi yao huko Sao Paulo, Septemba 5, 2021.
Nyota wa Brazil Neymar Jr na wa Argentina wanaongea kabla ya mechi yao huko Sao Paulo, Septemba 5, 2021. NELSON ALMEIDA AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashabiki waliweza kuangalia mechi hiyo kwa kipindi kisichozidi dakika 5, Jumapili (Septemba 5). Mamlaka ya afya ya Brazil iliingilia kati kusitisha mechi hiyo, ikibaini kwamba kulikuwa na uwongo kwa madai ya wachezaji wanne wa Argentina. Wanashtumiwa kukiuka itifaki ya afya kwa kuingia nchini Brazil bila kutaja kuwa waliingia nchini humo wakitokea Uingereza, bila hata hivyo kuwekwa karantini kwa siku 14, kulingana na hatua iliyochukuliwa nchini Brazil kwa wageni wote wanaowasili kutoka Uingereza.

Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, lililoshtushwa na tukio hilo, imesema "inasikitishwa" kusitishwa ghafla kwa mechi hiyo na kuahidi kuchukuwa "uamuzi" wa kinidhamu. Uamuzi huo utachukuliwa dhidi ya nani na kwa utaratibu gani? Hakuna anayejua bado.

Shirikisho la Soka Duniani, lililosimamia mechi hii ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022, lilmesemakusikitishwa na "tukio la kusitishwa" kwa mechi, "ambayo ilizuia mamilioni ya wafuasi kuangalia mechi kati ya mataifa mawili makubwa zaidi ya mpira wa miguu duniani ”. “Ripoti rasmi za kwanza za mechi zimetumwa kwa FIFA. Ripoti hii itachambuliwa na vyombo husika vya nidhamu na uamuzi utachukuliwa kwa wakati unaofaa, ”limeongeza shirikisho hilo la Soka Duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.