Pata taarifa kuu

Euro2020: Wanamichezo wakashifu vitendo vya ubaguzi wa mashabiki wa Uingereza

Wanasiasa nchini Uingereza pamoja na viongozi wa chama cha soka nchini humo FA, wameeleza kusikitishwa na vitendo walivyosema sio vya kiungwana, ambapo mashabiki wa soka nchini humo waliwaonesha vitendo vya ubaguzi wa rangi na matusi, wachezaji kadhaa wa kikosi cha taifa.

Kocha wa England, Gareth Southgate, amelaani vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji weusi kwenye timu yake baada ya kupoteza penati 3 dhidi ya Italia siku ya Jumapili, Julai 12, 2021
Kocha wa England, Gareth Southgate, amelaani vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji weusi kwenye timu yake baada ya kupoteza penati 3 dhidi ya Italia siku ya Jumapili, Julai 12, 2021 JOHN SIBLEY POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mbali na wachezaji Marcus Rashford, Jodan Sancho na Bukayo Saka, kutukanwa kupitia kwenye mitandao yao ya kijamii, bado mashabiki hao walifanya vurugu nje ya uwanja wa Wimbley, kwa kuwashambulia mashabiki wa Italia, ambao timu yao ilitawazwa kuwa mabingwa wa Ulaya.

 

Licha ya mtandao wa Facebook kudai kuwa utafuatilia matukio ya ubaguzi wa rangi kwenye mtandao wake wa Instagram, waziri mkuu Boris Johnson, amejikuta akikosolewa pakubwa kwa kushindwa kukemea vitendo vya mashabiki waliowazomea wachezaji wa Uingereza kwa kupiga goti kupinga ubaguzi wa rangi michezoni.

 

Mwanamfalme wa Uingereza, Prince William, nae kupitia ukurasa wake wa kijamii amewakashifu mashabiki waliotumia mitandao yao ya kijamii kuwatukana wachezaji hao watatu ambao walikosa mikwaju yao ya Penalt dhidi ya Italia.

 

Mbali na wanasiasa, chama cha soka nchini humo FA pamoja na wadau wachezaji wa zamani nchini Uingereza, wametoa kauli ya pamoja kulaani vitendo vya ubaguzi hasa vilivyofanywa na mashabiki wa Uingereza, kwa wachezaji iliyosema walipaswa kupongezwa kwa hatua waliyokuwa wamefikia.

 

Katika hatua nyingine, polisi na vyombo vingine vya usalama nchini humo, wamekosolewa kwa kushindwa kudhibiti usalama wakati wa mchezo wa fainali, hatua iliyoibua maswali kuhusu mpango wa nchi hiyo kuomba kuwa waandaaji wa mashindano ya koombe la dunia yam waka 2030.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.