Pata taarifa kuu
TENNIS

Djokovic ashinda taji la Wimbledon 2021

Novak Djokovic amefanikiwa kupata mataji 20 ya mashindano makubwa duniani, Grand Slam, katika mchezo wa Tennis, baada ya kushinda taji lake la sita la mashindano ya Wimbledon, mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Uingereza.

 Novak Djokovic bingwa wa mashindano ya Wimledon mwaka 2021. Julai 11 2021
Novak Djokovic bingwa wa mashindano ya Wimledon mwaka 2021. Julai 11 2021 Steven Paston POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Bingwa huyo wa dunia alimshinda Matteo Berrettini raia wa Italia kwa seti za 6-7 (4/7), 6-4, 6-4, 6-3 na ushindi huo sasa umempeleka kuwa na mataji sawa na wachezaji wenzake Roger Federer na Rafael Nadal.

Federer ameelezea ushindi wa Djokovic kama wa kipekee katika historia ya mchezo wa Tennis.

Mbali na taji hilo la Sita katika mashindano ya Wimbeledon, Djokovic raia wa Serbia ambaye ameshiriki kwenye fainali 30 za mashindano makubwa, ameshinda Australian Open mara tisa, Roland Garros mara mbili na US Open mara tatu.

Mbali na mataji hayo makubwa, Djokovic mwenye umri wa miaka 34 kwa ujumla ameshinda mataji 85 katika historia yake ya mchezo huo na anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda Dola Milioni 150 katika mchezo huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.