Pata taarifa kuu
SOKA-EURO 2020

Historia ya timu nne zilizofika hatua ya nusu fainali kuwania taji la bara Ulaya

Timu nne zilizofika katika hatua ya nusu fainali, kuwania taji la soka barani Ulaya, zipo kwenye maandalizi  ya mwisho kuelekea mechi ya kwanza siku ya Jumanne.

Timu ya taifa ya Uingereza baada ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la soka barani Ulaya
Timu ya taifa ya Uingereza baada ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la soka barani Ulaya Ettore Ferrari POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mechi zote za hatua hiyo, zitachezwza katika katika uwanja wa Wembley jijini London nchini Uingereza, sawa na fainali itayochezwa siku ya Jumapili.

Mchuano wa ufunguzi utakuwa kati ya Italia ambayo iliwahi kushinda taji hili mara moja mwaka 1968 na Uhispania ambayo imewahi kushinda taji hili mara tatu, mwaka 1964, 2008 na 2012.

Siku ya Jumatano, Uingereza nao watakuwa wanatupa karata yao dhidi ya Denmark, wakiwa na matumaini ya kufika katika fainali kubwa ya mchezo wa soka tangu iliponyakua kombe la dunia mwaka 1966.

Mwaka 1996 Uingereza pia ilifika katika hatua hii ya nusu fainali na matokeo mazuri ilipata mwaka 1968 ilipomaliza katika nafasi ya tatu.

Denmark nayo inakwenda katka mechi hii muhimu ikiwa na kumbukumbu ya kushinda taji hili mwaka 1992. Mwaka 1984 wakati michuano hii ilipofanyika nchini Ufaransa, ilifika pia katika hatua ya nusu fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.