Pata taarifa kuu
EURO 2020

Euro 2020: Ubelgiji yawaondoa mabingwa watetezi Ureno

Bao la kiungo mshambualiaji Thorgan Hazard katika dakika ya 42 kipindi cha kwanza, lilitosha kuipeleka Ubelgiji katika hatua ya robo fainali ya kutafuta ubingwa wa soka barani Ulaya, baada ya kuwaangusha mabingwa watetezi Ureno.

Thorgan Hazard baada ya kuifungia Ubelgiji bao muhimu 27 Juni  2021
Thorgan Hazard baada ya kuifungia Ubelgiji bao muhimu 27 Juni 2021 LLUIS GENE POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huo sasa umewafungulia milango ya kumenyana na Italia katika hatua hiyo ya robo fainali.

Licha ya ushindi huo majereha ya  Kevin De Bruyne na Eden Hazard,  yanaonekana kuzua wasiwasi kwenye kambi ya Ubelgi ambayo inasaka taji hilo.

Kocha Roberto Martinez anaamini, wachezaji hao wawili wanaotegemewa, watakuwa katika hali nzuri kabla ya mchuano wa robo fainali, Julai 2 mjini Munich nchini Ujerumani.

Aidha, amewasifu wachezaji wake kwa kuonesha kiwango cha juu cha mchezo na ukomavu wa akili na vipaji katika mechi hiyo muhimu.

Lakini swali kubwa linasalia iwapo, kikosi cha Ubeljigi ambacho kwa zaidi ya siku 1,000 kimeorodheshwa kuwa bora dunia, kitashinda mashindano ya bara Ulaya.

Wachambuzi wa soka wanasema kikosi cha sasa cha Ubelgiji, kinaweza kuitwa kikosi bora cha kizazi hiki.

 

Katika hatua nyingine, mshambualiji wa Ureno, Cristiano Ronaldo alijaribu kuitafutia timu yake  bao la kusawazisha bila mafanikio huku kipa wa Ubelgiji Thibaut Courtois  akimyima nafasi hiyo na sasa, ameondoka katika michuano hiyo akiwa na rekodi ya kuifungia nchi yake mabao matano.

Kikosi cha Ubelgiji kinachoshiriki kwenye michuano hii ni pamoja na:-

Thibaut Courtois,  Simon Mignolet , Mats Selz, Jan Vertonghen , Toby Alderweireld ,  Thomas Vermaelen , Dedryck Boyata , Jason Denayer,  Leander Dendoncker , Timothy Castagne ,  Thomas Meunier,  Kevin De Bruyne ,  Nacer Chadli , Yannick Carrasco , Youri Tielemans , Thorgan Hazard .

Wengine ni:-

Axel Witsel ,  Dennis Praet ,  Hans Vanaken ,  Dries Mertens ,  Romelu Lukaku , Christian Benteke ,  Michy Batshuayi ,  Eden Hazard, Jeremy Doku  na Leandro Trossard.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.