Pata taarifa kuu
EURO 2020-ROBO FAINALI

Euro 2020: Timu nane zitakazochuana hatua ya robo fainali zafahamika

Timu nane zitakazomenyana katika hatua ya robo fainali, kuwania taji la soka barani Ulaya zimefahamika baada ya kumalizika kwa hatua ya 16 bora siku ya  Jumanne usiku.

Nahodha  Harry Kane akisherehekea bao baada ya kuifunga Ujerumani katika mechi ya hatua ya 16, Juni  29 2021
Nahodha Harry Kane akisherehekea bao baada ya kuifunga Ujerumani katika mechi ya hatua ya 16, Juni 29 2021 Andy Rain POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ukraine na Uingereza zilikuwa timu mbili za mwisho kufuzu baada ya kupata ushindi katika mechi zao za mwisho za hatua ya mwondoano.

Uingereza ilikuwa ya kwanza kuingia katika hatua ya robo fainali siku ya Jumanne baada ya kuishinda Ujerumani mbaoa 2-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Wembley jijini London.

Raheem Sterling, aliipa Uingereza bao la ufunguzi katika dakika ya 75 ya mchuano huo, huku Harry Kane, akifunga bao la pili katika dakika ya 86.

Uingereza sasa itamenyana na Ukraine katika hatua ya robo fainali Julai 3.

 

Vikosi vya timu zote mbili:

Uingereza:  Pickford; Walker, Stones, Maguire; Trippier, Rice, Phillips, Shaw; Saka, Kane, Sterling

Ujerumani: Neuer; Ginter, Hummels, Rüdiger; Kimmich, Goretzka, Kroos, Gosens; Müller, Havertz, Werner

Ukraine nayo ilijikakamua na kuilaza Sweden mabao 2-1 na hii ndio mara ya Kwanza, inafika katika hatua hii.

Bao la ufunguzi la Ukraine lilifungwa na Oleksandr Zinchenko katika dakika ya 27 ya mchuano huo, huku Emil Forsberg akiisawazishia Sweden katika dakika ya 43 kabla ya timu zote kwenda kupumzika.

Kipindi cha pili, cha dakika 45 kilimalizika huku timu zote zikiendelea kuwa na matokeo ya sare, lakini Artem Dovbyk aliifungia Ukraine bao la pili katika dakika za ziada baada ya kupata bao la ushindi katika dakika ya 121.

 

Vikosi vya timu zote mbili:

Sweden: Olsen; Lustig, Lindelöf, Danielson, Augustinsson; S. Larsson, Olsson, Ekdal, Forsberg; Kulusevski, Isak

Ukraine: Bushchan; Karavaev, Zabarnyi, Kryvstov, Matviyenko; Sydorchuk, Stepanenko, Zinchenko; Yarmolenko, Yaremchuk, Shaparenko

Oleksandr Zinchenko  akisherehekea baada ya kuishinda Ukraine mabao 2-1 katika hatua ya 16 bora barani Ulaya.
Oleksandr Zinchenko akisherehekea baada ya kuishinda Ukraine mabao 2-1 katika hatua ya 16 bora barani Ulaya. Pool via REUTERS - PAUL ELLIS

Ratiba ya robo fainali:

Switzerland vs Uhispania- Julai 2 2021 katika uwanja wa Krestovsky jijini Saint Petersburg nchini Urusi.

Ubelgiji vs Italia- Julai 2 2021 katika uwanja wa Allianz Arena jijini Munich nchini Ujerumani.

Jamhuri ya Czech vs Denmark- Julai 3 2021  katika uwanja jijini Baku nchini Azerbaijan

Ukraine vs Uingereza- Julai 3 2021 katika uwanja wa Olimpico  jijini Rome nchini Italia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.