Pata taarifa kuu
AFRIKA-SOKA

CAF yathibitisha kuahirishwa kwa michuano ya Kombe la Dunia la 2022

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) ilikutana katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Mei 15. Uamuzi umechukuliwa kuhusu maadalizi ya michuano kababmbe katika bara hilo inayochezwa kila baada ya miaka miwili. 

Gianni Infantino, Paul Kagame na Patrice Motsepe huko Kigali, Rwanda, Mei 15, 2021.
Gianni Infantino, Paul Kagame na Patrice Motsepe huko Kigali, Rwanda, Mei 15, 2021. © Courtesy of CAF
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la CAF limethibitisha kuahirishwa kwa michuano ya ukanda wa Afrika kwa Kombe la Dunia la mwaka 2022: mechi zitapigwa mwishoni mwa mwaka 2021 na mwanzoni mwa mwaka 2022.

Mkutano uliofanyika Kigali Jumamosi hii ulivutia watu wengi. Paul Kagame, rais wa Rwanda, na Aurore Mimosa Munyangaju, Waziri wa Michezo wa Rwanda, wamempokea Gianni Infantino, rais wa FIFA, na Patrice Motsepe, rais mpya wa CAF, kwa mkutano wa Kamati ya Utendaji ya CAF ( COMEX). Katika hafla hii, Paul Kagame alisisitiza juu ya " ripoti kuhusiana na mpira wa miguu na maendeleo barani Afrika", imebaini taarifa ya CAF.

Kombe la Dunia 2022: Mechi za duru ya kwanza (hatua ya muondoano) zitasakatwa mweziSeptemba, Oktoba na Novemba 2021, kisha Machi 2022

Masuala kadhaa yalijadiliwa wakati wa mkutano huu huko Kigali. Suala kuhusu michuano ya ukanda CAF kwa Kombe la Dunia iliyopangwa kuchezwa nchini Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18, 2022 pia limejadiliwa. Kama ilivyotangaza RFI mwanzoni mwa mwezi Mei, hatua ya makundi ya michuano hii ya Afrika haitopigwa mwezi Juni. 2021. COMEX ilithibitisha kuahirishwa kwa michuano hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.