Pata taarifa kuu
AFCON-MISRI-CAF

Fainali za 32 za mataifa ya Afrika kuanza leo nchini Misri

Fainali za 32 za mataifa ya Afrika zinaanza leo nchini Misri kwa kushirikisha mataifa 24, ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.

Uwanja wa Kimataifa wa michezo wa Cairo, ambapo mechi ya ufunguzi baina ya Misri na Zimbabwe itachezwa leo usiku
Uwanja wa Kimataifa wa michezo wa Cairo, ambapo mechi ya ufunguzi baina ya Misri na Zimbabwe itachezwa leo usiku Signify
Matangazo ya kibiashara

Mataifa hayo yamegawanywa katika makundi sita yenye timu nne nne ambapo baada ya kutamatika kwa hatua ya makundi timu 16 zitafuzu kucheza hatua ya 16 bora.

Mchezo wa ufunguzi leo ni  baina ya wenyeji Misri dhidi ya Zimbabwe ambao utaanza saa tano usiku majira ya Afrika mashariki sawa na saa nne kwa saa ya Afrika ya kati.

Wageni mbalimbali mashuhuri wameshawasili nchini Misri kushuhudia sherehe na mchezo wa ufunguzi akiwemo rais wa Shirikisho la kandanda duniani FIFA, Gian Infantino, Katibu Mkuu wake Fatuma Samoura.

Aidha viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwemo rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi na waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Amollo Odinga watahudhuria tukio hilo.

Baadhi Dondoo muhimu

Ni fainali za 32 za Afrika tangu kuasisiwa kwa mashindano hayo mwaka 1957

Kwa mara ya kwanza mataifa 24 yatashiriki fainali hizo

Nchi za Burundim Mauritania na Madagascar zimefuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza katika historia

Tanzania inashiriki fainali hizo tangu ilipofanya hivyo mwaka 1980, fainali zilizofanyika nchini Nigeria.

Uganda ni taifa pekee la Afrika amshariki lililowahi kufika hatua ya fainali ya mashindano hayo, mwaka 1978 dhidi ya Uganda.

Misri imeshinda taji la Afrika mara saba na inanuia kushinda mara ya nane katika ardhi ya nyumbani.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.