Pata taarifa kuu
CAF-TANZANIA-UGANDA-AFCON

Zifahamu timu shiriki katika fainali za Afrika kwa vijana zinazoanza kesho nchini Tanzania

Fainali ya 13, kutafuta ubingwa wa taji la Afrika katika mchezo wa soka kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 inafungua milango yake siku ya Jumamosi, Aprili 14 jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Tanzania inaandaa kwa mara ya kwanza fainali za Afrika za vijana
Tanzania inaandaa kwa mara ya kwanza fainali za Afrika za vijana wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Mataifa nane pamoja na Tanzania, ambao ni wenyeji wanashiriki katika michuano hiyo.
 

Timu nne zitakazofika katika hatua ya nusu fainali, zitafuzu kucheza kombe la dunia nchini Brazil mwezi Oktoba.

Mbali na Tanzania, mataifa mengine yanayoshiriki ni pamoja na Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda na Angola.

Kundi A, Tanzania, Nigeria, Angola na Uganda.

Kundi B, Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal.

Historia-Kundi A

Tanzania

Serengeti Boys, ndio wenyeji wa michuano hii ya vijana.

Hii ni mara ya pili kwa timu hii kushiriki katika michuano hii, mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2017 nchini Gabon.

Tanzania haikufanya vema katika michuano ya mwaka 2017 na kuondolewa mapema katika hatua ya makundi.

Wanakwenda katika michuano hii wakiwa mabingwa wa taji la Vijana ukanda wa CECAFA, taji waliloshinda mwaka 2018.

Nigeria

The Golden Eaglets inacheza katika michuano hii mara tisa.

Imeshinda mara mbili mwaka 2001 na 2007.

Mwaka 2017, haikufuzu katika michuano hiyo, mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2015 ilipomaliza katika nafasi ya nne nchini Niger.

Miaka iliyoshiriki ni 1995, 1999, 2001, 2003, 2005, 2007, 2013, 2015 na 2019.

Angola

Inashiriki katika michuano hii mara nne.

Mara ya kwanza ilifuzu mwaka 1997, lakini pia ikarejea mwaka 1999 na 2017.

Miaka yote iliyoshiriki katika michuano hii, ilifika katika hatua ya makundi.

Timu hii pia inafahamika kwa jina la Palanquinhas.

Uganda

Imefuzu katika michuano hii kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hii

Ilifuzu mwaka 2018 kuwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuishinda Ethiopia mabao 3-1.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Uganda Moses Magogo, anaamini kuwa, Uganda itaonesha ubora katika soka la vijana.

Historia-Kundi B

Guinea

Hii ni mara ya saba kufuzu katika michuano hii.

Haijawahi kushinda taji hili lakini mwaka 1995, 2015 na 2017 ilimaliza katika nafasi ya tatu.

Inatarajiwa kuleta ushindani mkubwa katika kundi hili.

Cameroon

Mabingwa wa mwaka 2003, wakati michuano hiyo ilipofanyika nchini Swaziland.

Baada ya ushindi huo,The Indomitable Lions ilifuzu katika michuano ya kombe la dunia nchini Finland na kuondolewa katika hatua ya makundi.

Mara ya kwanza kushiriki katika michuano hii ya Afrika ilikuwa ni mwaka 1999 na hii ni michuano yake ya saba.

Morocco

Hii ni mara ya pili kufuzu katika michuano hii.

Mara ya kwanza ilikiwa ni mwaka 2013, walipokuwa wenyeji na kumaliza katika nafasi ya nne.

Iliwahi pia kufuzu kombe la dunia mwaka huo wa 2013, wakati michuano hiyo ilipofanyika katika nchi ya Falme za Kiarabu na kuondolewa katika hatua ya 16.

Senegal

Imerejea katika michuano hii kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki mara ya mwisho 2011 na kuondolewa katika hatua ya makundi.

Timu hii imekuja katika michuano hii, ikiwa na matumaini ya kufuzu katika kombe la dunia, lakini pia kushinda taji hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.