Pata taarifa kuu
CAF-QATAR-KOMBE LA DUNIA 2022

Ujumbe wa CAF wazuru Qatar, kutathimini maandalizi ya Kombe la dunia

Ujumbe wa Shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) umezuru nchini Qatar kujionea maandalizi ya nchi hiyo kuelekea fainali za Kombe la dunia za mwaka 2022.

Rais wa CAF Ahmad Ahmad akiwa na viongozi wa soka nchini Qatar
Rais wa CAF Ahmad Ahmad akiwa na viongozi wa soka nchini Qatar www.soka25east.com
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa CAF umeongozwa na rais Ahmad Ahmad na umekutana na rais wa Shirikisho la kandanda nchini Qatar (QFA) Sheikh Hamad bin Khalifa bin Ahmed Al Thani.

Mbali na kujadili kuhusu fainali za Kombe la dunia pia viongozi hao wamejadili kuhusu miradi mbalimbali soka inayotekelezwa na pande hizo mbili.

Mkutano huo ni utekelezaji wa makubaliano baina ya taasisi hizo mbili kuhusu maendeleo ya mchezo wa soka yaliyotiliwa saini mwaka 2015 wakati huo CAF ikiongozwa na Issa Hayatou.

Baadhi ya vipengele vilivyomo katika makubaliano hayo ni utawala, mafunzo ya makocha, matibabu katika mchezo wa soka, waamuzi, kuendelea soka la vijana na wanawake, ujenzi wa miundombinu ya soka, masoko na mawasiliano.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.