Pata taarifa kuu
CECAFA-KOMBE LA KAGAME-SIMBASC

Simba yasalim amri kwa Azam

Klabu ya Simba imekiri kuwa imepoteza kiuhalali mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya Azam.

Wachezaji wa SImba
Wachezaji wa SImba Goal.com
Matangazo ya kibiashara

Azam FC ilitwa ubingwa wa michuano hiyo kwa kuirarua Simba  mabao 2-1.

Kocha msaidizi wa wa Simba, Masoud Djuma amesema Azam ilicheza vizuri ikilinganishwa na kikosi chake.

"Tumekubali, wao walicheza vizuri na sisi tulijaribu lakini wenzetu walikuwa imara sehemu ya kiungo,"alinukuliwa kocha huyo baada ya mchezo

Hili ni taaji la pili kwa Azan katika kipindi cha miaka minne ambapo mara ya mwisho ilishinda taji hilo mwaka 2015.

Simba ilichukua ushindi wa pili na kujinyakulia dola 20,000 na Gor Mahia ambayo ilichukua ushindi wa tatu kwa kuifunga JKU mabao 2-0 imepata dola 10,000.

Mashindano hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka mitatu lakini je yamekuwa na tija kwa timu shiriki?

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.