Pata taarifa kuu
CECAFA-KOMBE LA KAGAME-SIMBASC

Musonye awashutumu viongozi wa Cecafa kwa kuua soka

Katibu Mkuu wa Baraza la vyama vya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Nicholaus Musonye amesema soka katika ukanda wa Afrika mashariki na kati linaporomoka kutokana na hujuma za viongozi.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye The Standard
Matangazo ya kibiashara

Musonye alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka katika mkutano na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, siku moja kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame jijini Dar es Salaam.

“Kuna sabotage, hujuma inafanywa na viongozi wa Cecafa, mnapanga jambo moja lakini wengine wanaamua jambo lingine na kuanzisha mashindano yao.Hatuwezi kufika,”amesema Musonye.

Alipohojiwa ikiwa yuko tayari kuwajibika kutokana na soka la ukanda huu kuporomoka, Kiongozi huyo amesema yuko tayari kuachia wadhifa wake ikiwa viongozi wa Cecafa watamtaka kufanya hivyo.

“Mimi sing'ang'anii, ni kweli niko Cecafa tangu mwaka 1998 lakini kuna kitu tumefanya, hata kesho niko tayari kuondoka kama nikiamuliwa kufanya hivyo,”

Akijibu tuhuma kuwa Cecafa ni chanzo cha kuporomoka kwa soka, Kaimu rais wa Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani amekiri uwepo wa changamoto kutokana na viongozi wa Cecafa kuwa na mitazamo tofauti kuhusu maendeleo ya soka.

Usikose kusikiliza makala ya Jukwaa la Michezo, Jumapili Julai, 1 ambapo utasikiliza kwa kina mahojiano na Katibu Mkuu wa Cecafa, baadhi ya timu shiriki na wadau wa soka

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.