Pata taarifa kuu
KENYA-SOKA

Kenya yapoteza nafasi nane katika orodha ya FIFA

Kenya imeshuka nafasi nane na sasa ni ya 113 duniani katika orodha ya mwezi Aprili iliyotolewa na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Kenya ikikabiliana na Zanzibar katika fainali ambayo Harambee Stars ilishinda kwa mabao 4-3 katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos
Kenya ikikabiliana na Zanzibar katika fainali ambayo Harambee Stars ilishinda kwa mabao 4-3 katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos cecafafootball.org
Matangazo ya kibiashara

Tanzania ambayo ni ya 137 imepiga hatua tisa juu huku Uganda ambayo ni ya 74 duniani, ikipanda nafasi nne.

Harambee Stars imeonekana kushuka baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Comoros na kufungwa mabao 3-2 na Jamhuri ya Afrika ya Kati, katika michuano ya Kimataifa ya kirafiki mwezi uliopita.

Tanzania nayo mwezi uliopita, iliifunga DRC mabao 2-0 kabla ya kufungwa na Algeria mabao 4-1 katika mchuano mwingine wa kirafiki.

Ushindi wa Uganda dhidi ya Sao Tome Principe na sare dhidi ya Ushelisheli, imewasaidia vijana hao wa kocha Sebastien Desabre kupiga hatua.

Ubora wa timu za taifa katika mchezo wa soka hutolewa kila mwaka huu.

Ukanda wa CECAFA :

Uganda – 74 (+4)

Kenya – 113 (-8)

Rwanda – 123 (-11)

Sudan – 126 (-9)

Tanzania – 137 (+9)

Ethiopia – 145 (-8)

Burundi – 145 (-3)

Sudan Kusini– 155 (-1)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.