Pata taarifa kuu
CAF

Droo ya mechi za klabu bingwa na shirikisho Afrika kuchezeshwa leo

Kamati ya mashindano ya vilabu ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF imekutana hapo jana jijini Cairo, Misri na kipitisha taratibu za kuchezesha droo ya hatua ya makundi ya michuano ya Klabu bingwa na ile ya michuano ya kombe la shirikisho.

Nembo za mashindano ya CAF
Nembo za mashindano ya CAF RFI Kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Droo hiyo inatarajiwa kuchezeshwa hivi leo katika ukumbi wa Ritz Carlton jijini Cairo maajira ya saa 12:00 jioni.

Timu zilizofuzu ziligawanywa kulinga na namna zilivyofanya kwenye makala tani za mwishi za mashindano ya vilabu ya CAF (2017, 2016, 2015, 2014, 2013).

Makundi manne yalitengenezwa kwaajili ya michuano ya klabu bingwa na ni kama ifuatavyo:

Pot 1: TP Mazembe (DR Congo), Al Ahly (Egypt), Etoile du Sahel (Tunisia), Wydad (Morocco)

Pot 2: Mamelodi Sundowns (South Africa), Zesco (Zambia), Esperance (Tunisia), ES Setif (Algeria)

Pot 3: MC Alger (Algeria), KCCA (Uganda), Horoya (Guinea), Mbabane Swallows (Swaziland)

Pot 4: Primero de Agosto (Angola), Township Rollers (Botswana), Difaa El Jadidi (Morocco), AS Port (Togo)

Droo itaanza kwa kundi namba 4 kwa mpira wa kwanza kuchukuliwa kutoka kundi A na droo nyingine itafanyika kuamia nafasi ya A1, A2, A3 au A4.

Utaratibu huohuo utarudiwa kwa kundi namba 3, 2 na 1 kumaliza upangaji wa makundi rasmi.

Kwa michezo ya kombe la Shirikisho ambalo timu zitacheza mechi za mtoano kabla ya kuingia hatua ya makundi na zenyewe zitapangwa kulinga na matokeo yao ya mashindano matano yaliyopita ambapo timu nne zilitolewa kutoka mashindano ya klabu bingwa zimewekwa kwenye pot A na timu nne za juu katika kombe la shirikisho zimewekwa Pot B.

Timu nyingine 12 zilizosalia kutoka mashindano ya klabu bingwa zimewekwa kwenye Pot C na nyingine kutoka mashindano ya shirikisho zimewekwa Pot D.

Pot A: El Hilal (Sudan), Saint George (Ethiopia), AS Vita (DR Congo), Zanaco (Zambia)

Pot B: USM Alger (Algeria), Supersport (South Africa), Hilal Obied (Sudan), Enyimba (Nigeria)

Pot C: ASEC Mimosas (Cote d’Ivoire), Mounana (Gabon), Young Africans (Tanzania), Williamsville (Cote d’Ivoire), Aduana (Ghana), Gor Mahia (Kenya), UD Songo (Mozambique), MFM (Nigeria), Plateau (Nigeria), Rayon Sport (Rwanda), Generation Foot (Senegal), Bidvest (South Africa)

Pot D: CR Belouizdad (Algeria), La Mancha (Congo), CARA (Congo), El Masry (Egypt), Niefang (Equatorial Guinea), Wolaitta Dicha (Ethiopia), Fosa Junior (Madagascar), Djoliba (Mali), RS Berkane (Morocco), Raja Club Athletic (Morocco), Costa do Sol (Mozambique), Akwa (Nigeria)

Droo ya kwanza itaamua mechi kati ya timu kutoka Pot A na Pot D na utaratibu huu utarudiwa mara nne.

Zoezi hili lilikamilika timu nane zilizobaki kutoka Pot C zitacheza nyumbani na ugenini kutoka Pot D na mpira mmoja kutoka Pot C utawekwa na mpira mwingine kutoka Pot D utaratibu huu utarudiwa mara 8 ili kupata ratiba kamili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.