Pata taarifa kuu
GOR MAHIA-SOKA

Meddie Kagere apata tuzo ya mchezaj bora ligi kuu ya Kenya

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Gor Mahia nchini Kenya Meddie Kagere ndio mchezaji bora nchini humo kwa mwaka 2017.

Meddie Kagere mchezaji bora wa soka nchini Kenya
Meddie Kagere mchezaji bora wa soka nchini Kenya citizen tv
Matangazo ya kibiashara

Tuzo hiyo ilitolewa na chama cha wanahabari wa michezo nchini humo SJAK.

Mchezaji huyo kutoka nchini Rwanda, aliisaidia klabu yake ya Gor Mahia kunyakua taji la ligi kuu kwa mara 16 kwa kufunga mabao 14 na kusaidia kufungwa kwa mabao 18.

Mwaka 2015, aliibuka katika nafasi ya pili mbele ya Michael Olunga ambaye siku hizi anacheza soka la kulipwa katika klabu ya Girona nchini Uhispania.

Mwaka 2016, mshindi alikuwa ni Kenneth Muguna ambaye pia ni mshambuliaji wa Gor Mahia.

Historia fupi ya Kagere:-

Kabla ya kusajiliwa na klabu ya Gor Mahia, aliwahi kuichezea KF Tirana ya Albania, Rayon Sport, Police FC, Kiyovu Sports na Atraco FC zote za  Rwanda.

Kagere mwenye umri wa miaka 31, pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Amavubi Stars.

Orodha kamili ya washindi:-

  • Mchezaji bora
  • Meddie Kagere

Kipa bora

  • John Oyemba – Kariobangi Sharks
  • David Juma- Kakamega Homeboyz
  • Patrick Matasi – Posta Rangers

Beki bora

  • Musa Mohammed – Gor Mahia
  • Jockins Atudo- Posta Rangers
  • Godfrey Walusimbi – Gor Mahia

Kiungo wa Kati

  • George ‘Blackberry’ Odhiambo – Gor Mahia
  • Lawrence Juma- Nzoia Sugar FC
  • Michael Madoya – Zoo FC

Mchezaji Chipukizi

  • Nicholas Kipkirui –Zoo FC
  • Vincent Oburu –AFC Leopards
  • Brian Otieno – Nzoia Sugar FC

Mfungaji bora

  • Masoud Juma – Kariobangi Sharks
  • Meddie Kagere – Gor Mahia
  • Kepha Aswani – Nakumatt FC
  • Jacques Tuyisenge – Gor Mahia
  • Stephen Waruru- Ulinzi Stars

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.