Pata taarifa kuu
URUSI 2018-ICELAND-KOSOVO

Iceland yafuzu Kombe la Dunia 2018

Timu ya taifa ya Iceland imefuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kuwacharaza Kosovo kwa mabao 2-0 na kumaliza wa kwanza katika kundi lao la kufuzu kwa michuano hiyo itakayopigwa nchini Urusi mwaka 2018.

Mashabiki wakiwapongeza wachezaji wao wa timu ya taifa ya Iceland.
Mashabiki wakiwapongeza wachezaji wao wa timu ya taifa ya Iceland. REUTERS/John Sibley Livepic
Matangazo ya kibiashara

Iceland ni nchi ya kwanza kufuzu kwa Kombe la Dunia ikiwa na idadi ya watu ambao ni chini ya milioni moja.

Iceland, ni taifa lenye wakazi 335,000 pekee. Mwaka 2016 katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ilifika robo fainali baada ya kuwaondoa Uingereza hatua ya 16 bora.

Bao la kwanza la Iceland lilifungwa na Gylfi Sigurdsson muda mfupi kabla ya mapumziko na bao la pili lilifungwa na Johann Gudmundsson na hivyo kuhakikishia kufuzu kwa timu hiyo kwa Kombe la Dunia 2018 nchini urusi.

Timu hii ya taifa ya Iceland imeshinda mechi saba kati ya 10.

Meneja wa Kosovo Albert Bunjaki amekaribisha ushindi wa Iceland kwa ushindi huo.

Meneja wa Iceland Heimir Hallgrimsson alisifu sana vijana wake akisema kwamba awali alikua na wasiwasi ya kupoteza nafasi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.