Pata taarifa kuu
SOKA-PSG-BARCA-NEYMAR-MCHEZO

Neymar anunuliwa kwa kitita cha euro Milioni 222

Hii ni rekodi katika historia ya soka. Klabu ya Ufaransa ya Paris Saint Germain ililipa euro Milioni 222 kwa kumnunua mshambuliaji nyota wa Barcelona Neymar kutoka Brazil.

Katika klabu ya PSG, mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar atalilipwa mshahara wa euro Milioni 30 kwa mwaka.
Katika klabu ya PSG, mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar atalilipwa mshahara wa euro Milioni 30 kwa mwaka. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Ununuzi huo wa mchezaji huyo wa miaka 25 umevunja rekodi ya awali iliyowekwa Paul Pogba aliporejea Manchester United kutoka Juventus kwa £89m Agosti 2016.

Neymar amenunuliwa kwa kitita kikubwa cha fedha ikilinganishwa na fedha zilizotolewa na Machester United kwa kumnunua Paul Pogba kutoka Juventus. Paul Pogba alinunuliwa euro Milioni 105,

Kititia hiki alichonunuliwa Neymar ni ada ya uhamisho inayomruhusu mchezaji huyu nyota wa Brazil kusitisha mkataba wake na Barcelona ambao ungemalizika mwaka 2021. Kitita hiki ambacho ni ada ya uhamisho kwa mchezaji huyu ni utaratibu uliodhinishwa na shirikisho la Soka nchini Uhispania.

Neymar atakuwa analipwa euro Milioni 45 kwa mwaka, na euro 865,000 kila wiki kabla ya kutozwa ushuru katika mkataba wake wa kwanza wa miaka mitano. Hiyo ni jumla ya Euro Milioni 450.

Neymar amesema amejiunga na mojawapo ya klabu zenye ndoto kuu zaidi barani Ulaya.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ufaransa imepanga kuwa na mkutano na waandisi wa habari leo Ijumaa saa 12:30 saa za Ufaransa.

Neymar baadaye atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wa PSG siku ya Jumamosi wakati wa mechi yao ya kwanza ya msimu mpya.

Neymar alifika kituo cha mazoezi cha Barcelona siku ya Jumatano akiandamana na babake na mwakilishi wake na kufahamisha klabu hiyo ya Uhispania kwamba angetaka kuondoka.

Neymar alijiunga na Barca mwaka 2013 na akashinda mataji mawili ya La Liga na moja la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.