Pata taarifa kuu
SOKA-KENYA

Rais wa zamani wa FKF akanusha madai ya kufuja fedha za Shirikisho

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Sam Nyamweya amekanusha madai ya kufuja fedha za Shirikisho hilo wakati alipokuwa uongozini kabla ya kuondolewa kwake mapema mwaka 2016.

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Kenya Sam Nyamweya
Rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Kenya Sam Nyamweya Stafford Ondego
Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa FKF, unamtuhumu Nyaweya kwa kuchukua Dola za Marekani 25,000 kutoka katika Akaunti ya fedha ya Shirikisho hilo.

Nyamweya amesema hajawahi kufuja fedha hizo zilizokuwa zimepangiwa kuimarisha soka vijijini katika eneo la Aberderes.

Pamoja na madai hayo, Halmashauri ya FKF imempata na kosa lingine la rais huyo wa zamani kulishtaki Shirikisho hilo katika Mahakama za kawaida nchini Kenya kinyume na utaratibu wa FIFA.

FKF inasema baada ya kubaini Nyamweya alihusika katika makosa hayo amefungiwa kushiriki katika maswala ya soka nchini humo kwa miaka 10.

Nyamweya amesema ameshangzwa na hatua hiyo na kusema, hana cha kupoteza kwa sababu alishastaafu kuongoza soka na haiwezi akatumikia marufuku hayo.

Hata hivyo, amesema atakwenda Mahakamani kumshatki rais wa FKF Nick Mwendwa kwa kumharibia jina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.