Pata taarifa kuu
LIGI KUU ENGLAND

Leicester City yafanya mazungumzo rasmi na kocha Roy Hodgson kuchukua mikoba ya Ranieri

Mabingwa la ligu kuu ya soka nchini Uingereza, klabu ya Leicester City, imeripotiwa kufanya mazungumzo rasmi na aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson, ili awe kocha mkuu mpya wa timu hiyo.

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson, mwenyesuti akitazama mchezaji wake Wyne Rooney wakati wa fainali za Euro 2016 nchini Ufaransa.
Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson, mwenyesuti akitazama mchezaji wake Wyne Rooney wakati wa fainali za Euro 2016 nchini Ufaransa. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 69 sasa, ni mmoja kati ya watu wanoatajwa sana kuchukua nafasi ya Claudio Ranieri aliyefutwa kazi na klabu hiyo wiki iliyopita.

Kuna taarifa pia, huenda kocha wa sasa wa mpito, Craig Shakespeare akasalia hadi mwishoni mwa msimu wa ligi ikiwa matokeo yataendelea kuwa mazuri.

Wakati huohuo aliyewahi kuwa kocha wa makipa wakati Hodgson akifundisha, Dean Kiely, amesema taarifa zinazoenea kwa uma kuhusu kocha huyo mkongwe sio sahihi na kwamba yeye ndiye anayepaswa kuwa mstari wa mbele kuchukua kibarua hicho.

Hodgson amekuwa nje ya uwanja bila kuwa na timu yoyote toka timu ya taifa ya Uingereza ilipotolewa kwenye michuano ya kombela mataifa ya Ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa.

Hodgson, ambaye amekuwa kocha kwa zaidi ya miaka 40, aliiongoza klabu ya Fulham kucheza fainali ya michuano ya Europa League mwaka 2012, na pia amekuwa kocha wa Liverpool na West Brom kabla ya kuchukua nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.