Pata taarifa kuu
CAF-SOKA

Fainali ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 kuanza Jumapili nchini Zambia

Makala ya 20 fainali ya mchezo wa soka kuwania taji la bara Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 inaanza kutifua vumbi siku ya Jumapili nchini Zambia.

Uwanja wa soka wa Levy Mwanawasa mjini Ndola
Uwanja wa soka wa Levy Mwanawasa mjini Ndola Yutube
Matangazo ya kibiashara

Michuano hii itachezwa katika uwanja wa taifa jijini Lusaka na ule wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, na kumalizika tarehe 12 mwezi Machi.

Mataifa yatakayoshiriki katika michuano hii ni pamoja na wenyeji Zambia, Sudan, Afrika Kusini, Senegal, Mali, Guinea, Misri na Cameroon.

Mataifa yatakayomaliza katika nne bora, yatafuzu kucheza katika michuano ya kombe la dunia nchini Korea Kusini mwezi Mei.

Mataifa yanayoshiriki katika michuano hii yamejumuisha katika makundi mawili.

Kundi la A:- Zambia, Guinea, Misri na Mali.
Kundi la B:- Senegal, Sudan, Cameroon na Afrika Kusini.

Mabingwa wa taji hili ni Nigeria walioshinda mwaka 2015.

Historia ya washindi wa taji hili:-

1.Nigeria imeshinda mara 7 mwaka-1983, 1985, 1987,1989,2005,2011 na 2015
2.Misri imeshinda mara 4 mwaka -1981, 1991, 2003, 2013
3.Ghana imeshinda mara 3, mwaka -1993,1999, 2009
4.Cameroon imeshinda mara 1 mwaka -1995
5.Algeria mara 1 mwaka -1979
6.Morroco mara 1 mwaka -1997
7.Angola mara 1 mwaka -2001
8.Congo mara 1 mwaka -2007
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.