Pata taarifa kuu
SOKA

CAF yataka Afrika kutengewa nafasi 10 michuano ya kombe la dunia kuanzia 2026

Bara la Afrika linataka uwakilishi wa mataifa 10 katika michuano ya soka ya kombe la dunia kuanzia mwaka 2026, wakati michuano hiyo itakapowashirikisha mataifa 48.

Rais wa Shirikisho la soka duniania FIFA, Gianni Infantino
Rais wa Shirikisho la soka duniania FIFA, Gianni Infantino Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mashirikisho yote ya soka barani Afrika yameunga mkono kuongezwa mara mbili kwa mataifa ya Afrika yanayoshiriki katika michuano hii.

Hili limebainika wakati wa Mkutano wa Baraza kuu la Shirikisho la soka duniani FIFA uliofanyika jijini Johannersburg nchini Afrika Kusini.

Bara la Ulaya nalo linataka uwakilishi wa timu 16 kutoka 13, lakini pia mataifa yao yasipangwe pamoja katika michuano ya hatua ya makundi.

Mataifa ya bara Asia nayo yanataka ushiriki wao kuongeze hadi mataifa nane au tisa kutoka manne wakati huu.

Mapendekezo haya yatatekelezwa tu ikiwa yatapitishwa na wajumbe wa Baraza kuu la FIFA.

Mwaka 2018 na 2022, mataifa yatakayoshiriki katika kombe la dunia yatasalia kuwa 32.

Kuongezwa kwa mataifa zaidi katika michuano hiyo, kulikubaliwa mwaka uliopita, baada ya kupendekezwa na rais wa FIFA Gianni Infatino kwa lengo la kuongeza ushiriki wa mataifa mbalimbli katika michuano hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.