Pata taarifa kuu
SOKA-CAF

Vlabu vya Afrika Mashariki na Kati vyafuzu mzunguko wa kwanza taji la klabu bingwa Afrika

Al-Merrikh ya Sudan, KCCA ya Uganda, AS Vita Club ya DRC na Yanga ya Tanzania zimefuzu katika mzunguko wa kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika mwaka 2017.

Nembo ya taji la klabu bingwa barani Afrika
Nembo ya taji la klabu bingwa barani Afrika Courtesy of CAF
Matangazo ya kibiashara

Vlabu hivi vilifuzu baada ya kumalizika kwa michuano ya marudiano hatua ya wali mwishoni mwa wiki iliyopita, zilizopigwa katika viwanja mbalimbali barani Afrika.

Michuano ya mzunguko wa kwanza, itachezwa mwezi Machi nyumbani na ugenini na mshindi atafuzu katika hatua ya makundi.

KCCA itamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambao ndio mabingwa watetezi wa taji hili, huku Rivers United ya Nigeria ikimenyana na Al-Merrikh ya Sudan.

Yanga ya Tanzania itamenyana na Zanaco ya Zambia. Zanaco ilifuzu baada ya kuishinda APR ya Rwanda katika hatua ya awali.

AS Vita Club nayo itatafuta nafasi ya kufuzu na itamenyana na Gambia Ports Authority huku TP Mazembe ya DRC ikimenyana na CAPS United ya Zimbabwe.

Ratiba nyingine ya michuano ya klabu bingwa:-

  • Al-Hilal vs AS Port-Louis 2000
  • AC Leopards vs Saint George
  • Al-Ahly vs Bidvest Wits
  • Coton Sport vs CnaPS Sport
  • Zamalek vs Enugu Rangers
  • Ferroviario Beira vs Stade Malien
  • Wydad Casablanca vs CF Mounana
  • Al-Ahli Tripoli vs FUS Rabat
  • Esperance de Tunis vs Horoya
  • Etoile du Sahel vs AS Tanda
  • USM Alger vs Rail Club du Kadiogo

Vlabu 16 vitafuzu katika hatua ya makundi na kugawanywa katika makundi manne, kila kundi na vlabu vinne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.