Pata taarifa kuu
CAF-SOKA

TP Mazembe na Mamelodi Sundowns kumenyana fainali ya CAF Super Cup

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka DRC na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zitashuka dimbani siku ya Jumamosi kupambana katika fainali ya kuwania taji la CAF Super Cup.

Wachezaji wa TP Mazembe katika mchuano muhimu uliopita mwaka 2016
Wachezaji wa TP Mazembe katika mchuano muhimu uliopita mwaka 2016 stringer / AFP
Matangazo ya kibiashara

Fainali hii ya kila mwaka, inawakutanisha mabingwa wa taji la klabu bingwa Afrika msimu uliopita ambao ni Mamelodi Sundowns and TP Mazembe walioshinda taji la Shirikisho barani Afrika.

Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria kuanzia saa mbili usiku saa za Afrika Mashariki.

Mazembe wanashiriki kwa mara ya tatu katika michuano hii baada ya kufanya hivyo mwaka 2010 na 2011.

Mamelodi itakuwa inamtegemea sana mshambuliaji wake Khana Billiant kutoka Zimbabwe huku Mazembe ikimtegemea sana nahodha mpya Rainford Kalaba raia wa Zambia.

TP Mazembe pia inakwenda katika mchuano hii ikiwa na kocha mpya Mfaransa Thierry Froger.

Mabingwa watetezi ni TP Mazembe ambao mwaka 2016, waliishinda Etoile du Sahel kwa mabao 2-1, fainali iliyochezwa katika uwanja wa Stade TP Mazembe mjini Lubumbashi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.