Pata taarifa kuu
RWANDA-SOKA

Makocha 52 waomba kazi ya kuifunza Amavubi Stars

Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA, limetangaza orodha ya makocha 52 wote raia wa kigeni walioomba kazi ya kuifunza timu ya taifa Amavubi Stars.

Makao makuu ya Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA
Makao makuu ya Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA www.ferwafa.rw
Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita, FERWAFA ilitangaza kuwa ilikuwa inamtafuta kocha kujaza nafasi ya Jonathan McKinstry ambaye alifutwa kazi baada ya matokeo mabaya mwaka uliopita.

Kocha mpya anatarajiwa kuindaa Rwanda kufuzu katika michuano ya CHAN mwaka 2018 nchini Kenya, lakini pia kufuzu katika michuano ya mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwaka 2019.

Miongoni mwa makocha walioomba kazi hiyo ni pamoja na aliyekuwa kocha wa Algeria George Leekens na aliyekuwa kocha wa Kenya Antoine Hey.

Wengine ni pamoja na Winfried Schafer, Samson Siasia, Dragomir Okuka, Tom Saintfiet, Peter Butler, Nikola Kavazovic, Sebastien Desabre, Goran Kopunovic, Didier Gomes da Rosa ,Engin Firat mionhini mwa wengine.

Orodha Kamili:-
Adyam Kuzyavez (Urusi), Antoine Hey (Ujerumani), Alberto Nieto Sandoval Loro (Uhispania), Antonio Flores (Spain), Bernard Simondi (Ufaransa), Daniel Breard (Ufaransa), Danilo Doncic (Bulgaria), Denis Doavec (Ufaransa), Denis Lavagne (Ufaransa), Didier Gomes da Rosa (Ufaransa), Engin Firat (Ujerumani/Uturuki), Ermin Siljak (Slovenia).

Fran Castano (Uhispania), Jasminko Velic (Ureno/Serbia), Joao Parreira (Ureno), Jose Rui Lopes Anguas (Ureno), Kevin Reeves (Uingereza), Luis Norton de Matos (Urenol), Mihail Stoichita (Romania), Seslija Milomir (Bosnia), Manuel Madurerira (Portugal), Marc Lelievre (Ubelgiji), Mircenia Rednic (Ubelgiji/Romania), Mourad Ouardi (Algeria), Nasser Sandjak (France).

Nikola Kavazovic (Serbia), Paul Put (Ubelgiji), Pea Fulvio (Italy), Peter Butler (Uingereza), Pierre-Andre Schurmann (Switzerland), Ricardo Nuno Perreira (Ureno), Salomon Yannick (Ufaransa), Samson David Unuanel (Nigeria), Scott Donnelly (US/Uingereza), Sebastian Desabre (Ufaransa).

Tom Saintfiet (Ubelgiji), Vaz Pinto (Ureno), Winfried ‘Winni’ Schafer (Ujerumani), Denis Goavec (Ufaransa, Dimitrir Vasev (Bulgaria), Ermin Siljak (Slovenia), Fabio Lopez (Italia), Goran Kopunovic (Serbia), Maor Rozen (Uruguay), Marinko Koljanin (Croatia), Meziane Ighil (Algeria).

Peters Guy (Ubelgiji), Raoul Savoy (Swiss/Uhispania), Rodolfo Zapata Antonia (Marekani), Samson Siasia (Nigeria), Dragomir Okuka (Bosnia and Herzegovina) and Georges Leekens (Ubelgiji).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.