Pata taarifa kuu
AFCON 2017

DRC yafuzu hatua ya robo fainali

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefankiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya mataifa bingwa inayoendelela nchini Gabon.

Wachezaji wa DRC wakisherehekea baada ya kufuzu hatua ya robo fainali
Wachezaji wa DRC wakisherehekea baada ya kufuzu hatua ya robo fainali Justin TALLIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ilikuja Jumanne usiku baada ya kuishinda Togo mabao 3-1 katika mchuano muhimu wa mwisho wa kundi C katika uwanja wa Port-Gentil.

DRC ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 29 kupitia mshambuliaji matata Junior Kabananga baada ya kuunganisha pasi safi kutoka kwa mchezaji mwenzake Chancel Mbemba.

Ndombe Mubele naye alifunga bao la pili katika kipindi cha pili cha mchuano huo katika dakika ya 54, lakini ilipofika dakika ya 69.

Togo ilipata bao lake kupitia Kodjo Fo-Doh Laba na kuwapa vijana wa kocha Claude Le Roy matumaini ya kurejea katika mchuano huo.

Hata hivyo, mambo yalikuwa mazuri mno kwa DRC katika dakika 80 baada ya Paul-Jose M'Poku kufunga mkwaju wa adhabu na kuwapa vijana wa Florent Ibenge bao la tatu.

Leopard sasa inasubiri kufahamu mshindi wa pili wa kundi D kati ya Mali, Ghana au Misri ili kupambana katika hatua ya robo fainali, ila dalili zote zinaonesha kuwa itakuwa ni Misri.

Matokeo haya yameleta furaha kubwa kwa mashabiki wa soka mjini Kinshasa, Lubumbashi, Goma huku mashabiki wakiwa na matumaini ya timu yao kunyakua taji hili nchini Gabon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.