Pata taarifa kuu
AFCON 2017

Wafahamu makocha wa timu zinazoshiriki michuano ya AFCON nchini Gabon

Mataifa 16 yaliyofuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka huu nchini Gabon, yapo katika maandalizi ya lala salama kabla ya kufunguliwa rasmi kwa michuano hiyo siku ya Jumamosi.

Uwanja wa Kimataifa wa  'Amitié jijini  Libreville.
Uwanja wa Kimataifa wa 'Amitié jijini Libreville. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandalizi haya yanaongozwa na makocha mbalimbali. Huu ndio wasifu wao kwa kifupi.

Claude Le Roy
Huyu ni kocha wa timu ya taifa ya Togo.
Raia huyu wa Ufaransa ana rekodi ya kuwa kocha mwenye uzoefu mkubwa katika michuano hii ya mataifa bingwa barani Afrika.
Le Roy mwenye umri wa miaka 68, ana historia ya kuiwakilisha mataifa mbalimbali katika michuano hii.
Kocha huyu amekuwa katika michuano hii akiwa kocha wa DRC, Ghana, Congo, Senegal, Mali, Tunisia na sasa Togo.

Herve Renard
Raia huyu wa Ufaransa amekuwa na historia ya kipekee katika michuano hii.
Renard mwenye umri wa miaka 48, ambaye kwa sasa ni kocha wa Morocco, amekuwa katika michuano hii mara sita.
Mwaka 2012, aliisaidia Zambia kunyakua taji hili lakini pia 2015, aliiongoza Ivory Coast kunyakua taji hili baada ya kusubiri taji hili kwa muda mrefu.
Mbali na Ivory Coast na Zambia, amewahi pia kuwa kocha wa Angola na kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ghana.

Michel Dusuyer
Huyu ni kocha wa Ivory Coast kuanzia mwaka 2015.
Ana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa anaisaidia nchi hii inatetea taji lake.
Kipa huyu wa zamani mwenye umri wa miaka 57, amewahi kuwa kocha wa Guinea kwa muda mrefu, kati ya 2002-2004,2010-2013 na 2014-2015.
Mbali na Guinea, aliwahi pia kocha wa Benin kati ya mwaka 2008-2010.

Paulo Duarte
Kocha huyu kutoka Ureno anarejea katika michuano hii akiwa na timu ya taifa ya Burkina Faso.
Kati ya mwaka 2008-2012 kocha huyu mwenye umri wa miaka 47, aliwahi pia kuifunza Burkina Faso kabla ya kwenda Gabon kwa mwaka mmoja kati ya mwaka 2012-2013.
Mara ya mwisho kwa Burkina Faso kushiriki katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2015 na kuondolewa katika hatua ya makundi.

Alain Giresse
Kocha wa Mali tangu mwaka 2015, lakini pia amewahi kuifunza nchi hii kati ya mwaka 2010-2012.
Kocha huyu mwenye umri wa miaka 64, raia wa Ufaransa, amewahi pia kuifunza Gabon kati ya mwaka 2006-2010 na Senegal kati ya mwaka 2013-2015.

Amvram Grant
Kocha wa Ghana, raia wa Israel mwenye umri wa miaka 61.
Hii itakuwa mara ya kwanza kuwa katika michuano hii ya bara Afrika.
Alianza kuifunza Ghana kuanzia mwaka 2014.

George Leekens
Kocha wa timu ya taifa ya Algeria, mwenye umri wa miaka 67 kutoka Ubelgiji.
Alipewa kibarua cha Algeria mwaka 2016 lakini pia aliwahi kuifunza nchi hiyo mwaka 2003.
Kati ya mwaka 2014-2015 aliwahi pia kuifunza Tunisia.

Florent Ibengé
Kocha wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ibenge mwenye umri wa miaka 55, ni kocha mwenyeji ambaye mwaka 2016, aliisaidia nchi yake kunyakua taji la CHAN nchini Rwanda.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ibenge kuongoza nchi yake katika michuano hii ya mataifa bingwa barani Afrika.

Callisto Pasuwa
Kocha wa timu ya taifa ya Zimbabwe.
Yeye pia ni kocha mzawa.
Kocha huyu wa zamani wa kikosi cha timu ya taifa chini ya umri wa miaka 23, atakuwa anaiwakilisha nchi yake kwa mara ya kwanza, katika michuano ya tatu ya AFCON.

Henri Camara
Kocha wa timu ya taifa ya Senegal.
Mchezaji huyu wa zamani wa timu ya taifa mwenye umri wa miaka 39, anaiongoza nchi yake kwa mara ya kwanza katika michuano hii.
Camara amekuwa akisema akishinda taji hili, ataonyoa rasta zake.

Milutin “Micho” Sredojević
Kocha wa timu ya taifa ya Uganda. Ameisadia Uganda kufuzu katika michuano hii kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Micho mwenye umri wa miaka 47, kushiriki katika michuano hii.
Alianza kuifunza Uganda Cranes mwaka 2013.
Kati ya mwaka 2011-2013 aliwahi kuifunza Rwanda.

Hugo Broos
Kocha wa timu ya taifa ya Cameroon mwenye umri wa miaka 64 ni, raia wa Ubelgiji.
Alianza kuifunza timu hii mwaka 2016.
Cameroon ndio nchi yake ya kwanza kufunza soka barani Afrika.

Héctor Cúper
Kocha wa timu ya taifa ya Misri.
Raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 61.
Alianza kuwa kocha wa Misri tangu mwaka 2015.
Hii ndio mara ya kwanza kufunza soka barani Afrika, na kuonekana katika michuano hii.

Baciro Candé
Kocha wa Guinea-Bissau.
Ni kocha mzawa mwenye umri wa miaka 68.
Amekuwa kocha wa muda mrefu sana kati ya mwaka 2001-2010 na kurejea tena mwaka 2016.

Henryk Kasperczak
Kocha wa timu ya taifa wa Tunisia. Ni raia wa Poland mwenye umri wa miaka 70.
Amerejea tena Tunisia baada ya kuifunza kati ya mwaka 1994-1998.
Mbali na Tunisia, amewahi pia kuifunza Cote d'ivoire, Morocco, Mali na Senegal.

José Antonio Camacho
Kocha wa timu ya taifa ya Gabon.
Raia wa Uhispania mwenye umri wa miaka 61.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.