Pata taarifa kuu
SOKA-CAF

Nigeria, Ghana na Cameroon zaanza vizuri michuano ya wanawake barani Afrika

Cameroon na Afrika Kusini zitachuana siku ya Jumanne katika mchuano wa pili hatua ya makundi kutafuta bingwa wa makala ya 12 ya michuano ya Afrika katika mchezo wa soka kwa upande wa wanawake.

Cameroon ikisherehekea baada ya kuifunga Misri 2-0  katika mchuano wa ufunguzi kutafuta taji la Afrika kwa wanawake Novemba 19 2016.
Cameroon ikisherehekea baada ya kuifunga Misri 2-0 katika mchuano wa ufunguzi kutafuta taji la Afrika kwa wanawake Novemba 19 2016. cafoline
Matangazo ya kibiashara

Wenyeji wa michuano hii ambao ni Cameroon, walianza vizuri mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya kuishinda Misri mabao 2-0 katika mchuano wa ufunguzi, uliochezwa katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde.

Cameroon ilipata mabao yake kupitia mshambuliaji Gabrielle Onguéné katika dakika ya 25 kipindi cha kwanza huku, Christine Manie akifunga penalti katika dakika ya 72.

Ushindi huo unawafanya wenyeji kuongoza kundi hilo kwa alama tatu, wakifuatwa na Afrika Kusini na Zimbabwe ambao wana alama moja baada ya kutoka sare ya kutofungana katika mchuano mwingine wa kundi A.

Zimbabwe na Misri nao watamenyana siku ya Jumanne, huku wenyeji wakitaka ushindi ili kufuzu katika hatua ya mwondoano lakini Misri ikitafuta ushindi wake wa kwanza katika michuano hii.

Nao mabingwa watetezi wa taji hili Nigeria, walianza vema baada ya kuwafunga Mali mabao 6-0.

Mshambuliaji Asisat Oshoala anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya wanawake ya Arsenal nchini Uingereza, alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kuifuingia timu yake mabao manne, katika dakika ya 41,64, 69 na 78.

Mabao mengine ya Super Falcons wanaotafuta taji la nane katika historia ya michuano hii, yalitiwa kimyani na Francisca Ordega na Esther Sunday aliyefunga mkwaju wa penalti.

Nigeria wakimenyana na Mali katika mchuano wa kwanza wa kundi B, Novemba 20 2016
Nigeria wakimenyana na Mali katika mchuano wa kwanza wa kundi B, Novemba 20 2016 cafonline

Nigeria wanaongoza kundi la B kwa alama 3 mbele ya Ghana ambao pia wana alama tatu baada ya kuwafunga Kenya mabao 3-1.

Harambee Starlets ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 23 kupitia Essie Akida, ushindi ambao Kenya walifanikiwa kudhibiti kufikia wakati wa mapumziko.

Hata hivyo, mambo yalibadilika kipindi cha pili wakati Black Queens waliporejea kwa nguvu na kusawazisha katika dakika ya 50 kupitia Samira Suleman.

Mambo yalikuwa mabaya zaidi katika dakika ya 72, wakati Elizabeth Addo alipowashinda mabeki wa Kenya na kupachika bao la pili, kabla ya kufanya hivyo tena katika dakika ya 91.

Kenya na Ghana zikimenyana katika mchuano wa ufunguzi wa mechi ya kundi B, Ghana ilishinda kwa mabao 3-1
Kenya na Ghana zikimenyana katika mchuano wa ufunguzi wa mechi ya kundi B, Ghana ilishinda kwa mabao 3-1 cafonline

Hata hivyo, mashabiki wa Kenya wamemlamikia refarii wa mchuano huo kwa kuegemea upande wa Ghana.

Kenya ambayo inashiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza ni ya tatu katika kundi hili, huku Mali ikiwa ya mwisho.

Ratiba ya kundi B siku ya Jumatano Novemba 23

  • Nigeria vs Ghana
  • Kenya vs Mali
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.