Pata taarifa kuu
SHANGHAI MASTER-MURRAY

Murray atwaa taji la Shanghai Master, amsogelea Djokovic

Muingereza Andy Murray amefanikiwa kumfunga Roberto Bautista Agut kwa seti mbili bila na kutwaa taji la Shanghai Master, taji ambalo linamfanya amsogelee kwa karibu zaidi bingwa namba moja wa mchezo huo duniani Novak Djokovic.

Muingereza Andy Murray.
Muingereza Andy Murray. Reuters/Aly Song
Matangazo ya kibiashara

Murray ambaye hakuanza seti ya kwanza vizuri, alirejea kwenye mchezo dakika chache baadae na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa matokeo ya seti 7-6 na 6-1, dhidi ya Muhispania Bautista anayeshika nafasi ya 19 kwa ubora duniani.

Bautista alitinga kwenye hatua ya fainali baada ya kumfunga mchezaji nambari moja kwa mchezo huo, Novak Djokovic katika hatua ya nusu fainali.

Ushindi huu unamfanya Murray kuendelea kupata mafanikio katika mashindano aliyoshiriki mwaka huu, ambapo hili linakuwa ni taji lake la 6.

Murray mwenye umri wa miaka 29, yuko nyuma kwa alama 915 dhidi ya mpinzani wake Djokovic, akiongeza matumaini ya kumaliza kwenye nafasi ya kwanza kidunia, mwisho wa mwaka huu.

Hii ni mara ya tatu kwa Andy Murray kutwaa taji la michuano ya Shanghai Master, ambapo linamfanya ajikusanyie alama elfu 1.

Murray ambaye pia alishinda taji la China Open, October 9 mwaka huu, sasa anafanikiwa kushinda seti zake zote 23 katika mashindano mawili yaliyopita na hivi karibuni kwenye michuano ya Davis Cup.

Hata hivyo Murray hakuonekana kujinasibu sana au kujipa matumaini makubwa ya kushika namba moja ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, kwa kile anachosema anaamini pia, Djokovic atashinda baadhi ya mechi na kujiongezea alama zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.