Pata taarifa kuu
DAVIS CUP-TENESI

Argentina kucheza fainali ya tenesi ya Davis Cup, Uingereza kujiuliza tena

Timu ya mchezo wa tenesi ya Argentina imefanikiwa kuwatupa nje mabingwa watetezi wa taji la michuano ya Davis Cup, timu ya Uingereza kwa kuwafunga kwenye mchezo wa nusu fainali kwa seti 3-2 na kupata nafasi ya kucheza hatua ya fainali.

Mchezaji wa Argentina, Leonardo Mayer akishangilia akiwa na wachezaji wenzake baada ya kumfunga Muingereza Dan Evans.
Mchezaji wa Argentina, Leonardo Mayer akishangilia akiwa na wachezaji wenzake baada ya kumfunga Muingereza Dan Evans. Reuters / Andrew Boyers Livepic
Matangazo ya kibiashara

Uingereza ilipoteza kwa seti 2-0 katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo mjini Glasgow, lakini ushindi mara mbili wa siku ya Jumamosi ulifuatiwa na ushindi wa mchezaji mmoja mmoja wa Uingereza Andy Murray siku ya Jumapili.

Mchezaji Dan Evans alishinda seti ya kwanza iliyokuwa muhimu kuamua mshindi lakini mchezaji Leonardo Mayer alipambana na kurejea mchezoni na kushinda kwa seti 4-6, 6-3, 6-2 na 6-4.

Wachezaji wa Argentina sasa watasafiri kuelekea Croatia ambako ndiko mchezo wa fainali utapigwa mwezi November.

Hii ni mara ya tano kwa timu ya Argentina kufika kwenye hatua ya fainali ambapo watakuwa wanajaribu kushinda taji hili kwa mara ya kwanza.

Uingereza ambayo ilishinda taji hili ;a Davis Cuo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 79, miezi 10 iliyopita, itawalazimu kushinda mchezo wao wa Jumatano ili kuona ni timu gani watapambana nayo kwenye msimu wa mwaka 2017 mwezi February.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.