Pata taarifa kuu
RIO OLIMPIKI 2016

Van Wiekerk aweka rekodi mpya mita 400, Bolt, Murray wajinyakulia medali ya dhahabu

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, amefanikiwa kuweka rekodi ya tatu mfululizo kwa kushinda mbio za mita 100, huku mchezaji wa tenesi Muingereza Andy Murray akiipatia nchi ya Uingereza medali ya tano ya dhahabu, ikiwa ni mafanikio makubwa kwa timu ya Uingereza.

Bingwa wa dunia wa mbio za mita 400, raia wa Afrika Kusini, Wayde va Niekerk akiwa kando ya bango linaloonesha muda aliotumia kukimbia na kuweka rekodi.
Bingwa wa dunia wa mbio za mita 400, raia wa Afrika Kusini, Wayde va Niekerk akiwa kando ya bango linaloonesha muda aliotumia kukimbia na kuweka rekodi. REUTERS/David Gray
Matangazo ya kibiashara

Medali hii ya 15 ya dhahabu kwa timu ya Uingereza, unaifanya nchi hiyo kuwa ya pili kwenye orodha ya jedwali la medali, kufuatia ushindi wa mcheza sarakasi Max Whitlock na Justin Rose aliyeshinda kwenye mchezo wa Gofu.

Mwendesha baiskeli Jason Kenny alimshinda muingereza mwenzake Callum Skinner kushinda medali yao ya tano.

Bolt mwenye umri wa miaka 29 alimaliza mbio za mita 100 kwa muda wa sekunde 9.81 akimshinda Mmarekani Justin Gatlin, akihitimisha ubingwa wake katika mbio za Beijing mwaka 2008 na London mwaka 2012.

Usain Bolt, bingwa wa mbio za mita 100 kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016
Usain Bolt, bingwa wa mbio za mita 100 kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016 REUTERS/Gonzalo Fuentes

Bolt bado anabakiza mbio za mita 200 na zile za 4x400 relay, huku mwenyewe akisema kuwa "nilitarajia kwenda kasi zaidi lakini nimefurahi kushinda, niko hapa kuonesha uwezo na nimefanya kile nilichopaswa kukifanya." alisema Bolt.

Mwanariadha wa Afrika Kusini, Wayde van Niekerk alifanikiwa kuvunja rekodi ya dunia iliyowekwa na Michael Johnson kwa sekunde 1.15 wakati aliposhinda mbio za mita 400 na kushinda medali ya dhahabu kwa kutumia muda wa sekunde 43.03, rekodi iliyokuwa imekaa kwa siku elfu 6 na 198.

Andy Murray, mshindi wa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016
Andy Murray, mshindi wa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016 Reuters/Kevin Lamarque

Katika tenesi, bingwa wa michezo ya Olimpiki, Muingereza Andy Murray alifanikiwa kutetea taji lake baada ya kufanikiwa kumshinda Muargentina Juan Martin del Porto kwa seti 7-5 4-6 6-2 7-5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.