Pata taarifa kuu
SOKA-CECAFA

Ethiopia, Tanzania zaungana na Kenya katika hatua ya nusu fainali taji la CECAFA

Timu za taifa za soka za Ethiopia na Tanzania zimeungana na Kenya katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la  CECAFA kwa upande wa wanawake.

Rwanda ikimenyana na Ethiopia katika mchuano muhimu wa CECAFA Septemba 14 2016
Rwanda ikimenyana na Ethiopia katika mchuano muhimu wa CECAFA Septemba 14 2016 www.soka25east.com
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Ethiopia inayofahamika kama Lucy, ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuifunga Rwanda mabao 3-2 katika mchuano muhimu uliopigwa katika taasisi ya Njeru mjini Jinja nchini Uganda Jumatano jioni.

Wachezaji wa Ethiopia, walionesha kiwango cha kuvutia uwanjani wakicheza pasi fupifupi na kuwafurahisha mamia ya mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchuano huo.

Mabao ya Ethiopia yalifungwa na Sisaya Shetaye, Girma Berktawit na Losa Abera huku Gloria Sifa Nibagwire na Mukeshimana Dorothy wakiifungia Rwanda.

Michuano ya hatua ya makundi inamalizika siku ya Alhamisi kwa Kenya kumenyana na Zanzibar, huku mchuano mwingine muhimu wa kuamua ni nani atafuzu katika hatua ya nusu fainali ikiwa ni kati ya wenyeji Uganda na Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.